Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet
Maselle wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati wakikagua
maendeleo ya ujenzi wa vivuko vya Bugorola Ukara na Chato Nkome katika
tukio lilofanyika katika yadi ya Songoro. Ujenzi wa vivuko hivyo
unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, ujenzi huo
umechelewa kukamilika kama ilivopangwa kutokana na kutokea kwa ugonjwa
wa mafua makali maarufu Covid 19. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza
Mhandisi Hassan Karonda na kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro
inayojenga vivuko hivyo Major Songoro.





PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...