Na  Said Mwishehe,Michuzi TV

VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri,makatibu wakuu ,wakuu wa idara,maofisa, watumishi wa umma pamoja na mamia ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wameendelea kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu mzee Benjamin Mkapa.

Shughuli za kuaga mwili wa mpendwa wetu, Mzee Mkapa zilianza jana Jumapili na zinaendelea leo  Jumatatu na kumalizika kesho Jumanne ambayo ndio siku ya kuaga kitaifa.

Kwa siku ya leo, mbali ya wananchi kujitokeza na kutoa heshima zao za mwisho kwa mzee Mkapa, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas alitoa ratiba kuwa mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu, wakuu wa idara, watumishi, viongozi wa dini, wanahabari nao ni vema wakaitumia siku ya leo kumuaga mzee wetu.

Dk.Abbas alisema lengo ni kuifanya siku ya kesho ambayo itakuwa ya kitaifa kutoa nafasi kwa viongozi wakuu wa kitaifa,pamoja na wageni wengine nao kutoa heshima ya mwisho hasa kwa kuzingatia siku ya kesho itakuwa na matukio mengi.

Kutokana na ratiba hiyo tangu asubuhi ,viongozi na watumishi wameebdelea kuaga huku kwa upande wa wananchi kukiwa na msusuru mrefu wa foleni.Tangu asubuhi hadi muda huu mamia kwa mamia ya nchi wameendelea kuaga.

Utararibu nzuri uliopo Uwanja wa Uhuru umefanya kila mwananchi anayefika kutoa heshima za mwisho kwa mzee Mkapa anapata fursa hiyo na hivyo kufanya watu wengi kuaga.Kuna uzio ambao umewekwa kwa ajili ya kuhakikisha wanaokwenda kuaga wanapita kwa kufuata utaratibu na kisha kwenda mpaka ulipo mwili wa mzee Mkapa kutoa heshima ya mwisho.

Pia wapo baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali wastaafu ambao nao wamefika uwanjani hapo kwa siku ya leo na kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye anatarajiwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Jumatano ya Julai 29, huko kijijini kwake Lupaso.

Wakati huo huo kesho Jumatano, ambayo ndio itakuwa siku ya kitaifa kuaga mwili wa mpendwa wetu,Rais Dk.John Magufuli anatarajiwa kuongoza waombolezaji katika kutoa heshima ya mwisho ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania watahudhuria.















 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...