NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini,mkoani Pwani kimeungana na watanzania
wote kumkumbuka marehemu Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkàpa
na kusema kitaendelea kumkumbuka kwa utawala wake wa UWAZI na UKWELI.
Mwenyekiti
wa chama hicho ,Maulid Bundala anaeleza ,pia Mkapa atakumbukwa kwa
kupiga vita rushwa ,mchapakazi ,mwenye maono ambae kizazi cha sasa
kitakwenda kumkumbuka na kumuenzi nayo.
"Ni
mkombozi wa wanyonge kwani alipenda kila mmoja aishi kwa amani bila
kuonewa ,kutendewa haki ,na alikuwa mshauri na mwanadiplomasia mzuri "
alisema Bundala .
Nae mkazi wa Mailmoja ,Neema Lucas anaeleza Mkapa ametulea vizuri na ameimarisha amani na upendo kwa Watanzania .
Alikuwa
mpenda Uwazi na Ukweli katika utendaji kazi ,maadili kazini ,alipigania
kila mmoja afanye kazi ili kujiendesha kimaisha .
Mkazi
mwingine Patrick Namahuta, anafafanua kwamba , atamkumbuka Mkapa kwa
kuondoa kodi ya kichwa kwani aliweza kupambana na kuondoa kodi ya kichwa
na kuomba wananchi waendelee kumuenzi kwa kusoma kitabu cha maisha yake
ambacho amekitunga mwenyewe kabla ya umati wake .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...