Mkuu
wa wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera (aliyevaa kofia katikati) akiwa na
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Busega Bw. Anderson
Njiginya Kabuko (wa mbele kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea miradi
ya mendeleo iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya
Busega.
************************************
Wananchi watakiwa
kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na
serikali. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera
wakati wa ziara ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Busega
ilipotembelea miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na
serikali wilayani Busega.
Mhe. Tano Mwera
amewataka wananchi kuwa na mwamko katika miradi mbalimbali inayoletwa na
serikali wilayani Busega, kwani kufanya hivyo ni dhahiri kwamba
wananchi wamependezwa na ujio wa maendeleo wilayani Busega. Amewataka
mwananchi wasimame katika nafasi zao ili kuhakikisha miradi inasimama na
kumalizika kwa wakati.
Mhe. Mwera
amesisitiza kama wananchi wanatakiwa kushiriki kupitia nguvu kazi basi
washiriki ipasavyo, na kama watatakiwa kuchangia basi pia wafanye hivyo
kwa miradi inayohitaji ushiriki wao. Aidha amewaomba viongozi ngazi ya
vijiji kuhamasisha wananchi kushirki miradi mbalimbali kwani miradi hiyo
imeletwa kwaajili yao hivyo hawana budi kuipokea kwa mikono miwili hii
itachangia serikali kutaka kuleta miradi mingi Zaidi.
Katika ziara hiyo
miradi mbalimbali ilitembelewa ikiwemo ujenzi wa jengo la Utawala la
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule
za msingi na sekondari, ujenzi wa majengo kwenye zahanati, ujenzi wa
nyumba za watumishi na ujenzi wa miundombinu kwenye Hospitali ya Wilaya
ya Busega huku kamati ya ulinzi na usalama ikiridhishwa na utekelezaji
wa miradi hiyo.
Kwa upande
mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega,
Anderson N. Kabuko ameongeza kwamba miradi ambayo imetekelezwa ni juhudi
za watendaji ambao wamekuwa na utendaji mzuri matokeo yake ni
kukamilika kwa wakati miradi mbalimbali, lakini pia amesisitiza miradi
inayoendelea na utekelezaji wake itakamilika kwa muda uliopangwa.
Wilaya ya Busega
imetekeleza na inaendelea na utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo
ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Baadhi ya
wakazi wa Wilaya ya Busega wanafurahishwa na kasi ya maendeleo na kuomba
serikali kuleta miradi mingi zaidi ili maendeleo yawe ya haraka zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...