Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mh. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua semina ya siku tatu ya waratibu wa Uchaguzi, wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na maafisa Uchaguzi kutoka Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida inayofanyika Jijini Dodoma.
Balozi Omari Ramadhani Mapuri alisema, wasimamizi hao wa uchaguzi katika Kanda ya Kati wanatakiwa kuzingatia maadili wanapofanya kazi hiyo. Mafunzo ya siku tatu jijini hapa yaliyokutanisha washiriki 162, pamoja na Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mh. Balozi Omari Ramadhani Mapuri.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni Rasmi
Washiriki wakijaza fomu maalum kabla ya kula kiapo mbele ya Hakimu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Dodoma, Mary Senapee akiwaongoza wasimamizi wa uchaguzi Mkuu kutoka kanda ya Kati kula kiapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...