Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.

Shirika la viwango Tanzania TBS linaendelea kutoa mafunzo maalumu ya ujasiriamali na umuhimu wa ubora wa bidhaa kwa wajasiriamali Mkoani Kagera katika Semina Maalum Wezeshi ya kuwafanya Wajasiriamali hao bidhaa zao kukfikia matakwa ya Viwango.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amelishukuru shirika hilo kwa kuamua kuwafikia wajasiliamali kwenye maeneo yao na kuweza kuzijua changamoto zao katika usindikaji wa bidhaa zao.

Mafunzo hayo yamefanyika julai 27,mwaka huu katika ukumbi wa Bukoba hotel ambayo yamewahusisha wajasiliamali Zaidi ya 50 kutoka wilaya za mkoa huo ambapo wajasiliamali hao wameelezwa umuhimu wa kuwa na alama ya ubora(TBS)  kwenye bidhaa zao.

Kinawiro amesema kuwa wajasiriamali ni watu muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa ambao wanatakiwa kusaidiwa kwa kupewa elimu ya ujasiriamali pamoja na namna bora ya utunzaji wa bidhaa tangu zikiwa malighafi hadi kufikia hatua ya kwenda sokoni.

“Wajasiriamali ni watu muhimu kwa taifa letu, TBS mnalo jukumu kubwa sana la kuhakikisha wadau hawa wanapata elimu sahihi na bora yenye lengo la kuwainua katika shughuli zao, tunaona sasa nchi yetu imefikia uchumi wa kati mchango wa watu hawa upo mkubwa.” Ameeleza Kinawiro.

Ameongeza kuwa mkoa wa Kagera unapakana na nchi takribani nne ambazo zinaweza kuwa fursa kwa wajasiliamali wa mkoa huo hivyo wajasiriamali wakikosa alama za ubora kwenye bidhaa zao watakosa masoko kwenye nchi hizo kwakuwa zitakuwa hata hazitambuliki hata kama ni nzuri.

Aidha Kinawiro amewataka SIDO na TBS kuwasaidia wajasiriamali kupata vifungashio bora ili kuweza kuuza bidhaa zao kwa usafi na ubora na pia waweze kupata faida ambapo amesema kuwa changamoto hiyo imekuwa kero na kuwafanya wajasiriamali kutumia vifungashio vivyobora na kuwapelekea walaji kushindwa kununua bidhaa zao.

Akitaja lengo la Mafunzo hayo na Niaba ya Mkurugenzi, Meneja wa mafunzo na Utafiti kutoka TBS Bwn. Hamisi Sudi ni meneja utafiti na mafunzo kutoka TBS amesema kuwa  mafunzo Kama hayo yamekuwa yakitolewa mara kawa mara kwa wajasiriamali Nchini ili kuwawezesha wajasiriamali hao kuzalisha bidhaa zenye ubora kulingana na  ushindani kwenye soko la Dunia, na kuwaunia Kiuchumi kwa Kujipatia kipato kizuri, na hivyo Shirika linaendelea kuwasaidia wajasiriamali wote Nchini waweze kuzalisha bidhaa Bora,  na kupatiwa alama ya ubora (TBS) kwenye bidhaa zao ili kumfanya mlaji wa mwisho kuiamini bidhaa hiyo kutokana na uwepo wa alama hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuanza kuzalisha bidhaa zenye ubora Zaidi na kuweza kupata masoko makubwa.

Matungwa Daniel ni mkurugenzi wa kiwanda cha Nyaka Food kilichopo Manispaa ya Bukoba ambaye amesema kuwa amekuwa akipata changamoto ya kuuza bidhaa zake nje ya nchi kutokana na bidhaa zake kutokuwa na alama ya ubora (TBS) suala linalompelekea kukosa masoko licha ya kuwa watu kutoka nchi za nje wanazipenda bidhaa zake.

Ameongeza kuwa serikali ikiwasaidia wajasiliamali hao kupata alama ya ubora kwa haraka itawasaidia kupata masoko na kupunguza usumbufu kwao pale wanapokwenda kuuza bidhaa hizo.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiangalia bidhaa Unga Lishe kutoka Aggy Star watengenezaji wa Lishe na Virutubisho, wakati wa Semina ya mafunzo ya kufikia Viwango Mkoani Kagera.
Meneja Mafunzo na Utafiti kutoka TBS, Hamisi Sudi  akiwasilisha Hotuba ya Mkurugenzi mbele ya Wajasiriamali (hawapo pichani) yaliyofanyika Katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Hotel.
Afisa Viwango kutoka TBS, Zena Issa  akiwasilisha mada yake ya Vifungashio kwa Wajasiriamali wa Mkoa Kagera wakati wa Semina ya Mafunzo yaliyofanika Katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Hotel.
Baadhi ya Wajasiriamali  Mkoani Kagera wakiendelea kufuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na TBS Katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Hotel.
Baadhi ya Bidhaa zilizoletwa na Wajasiriamali katika Semina ya mafunzo ya TBS Mkoani Kagera zikionekana Juu ya meza Kama zilivyoletwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...