Viongozi
mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wameanza kuwasili nchini kuhudhuria
maziko ya kitaifa ya Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia
ijumaa ya Julai 24,2020 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni amekuwa kiongozi wa
kwanza kutoka mataifa ya nje kuwasili hapa nchini majira ya saa tano na
dakika 20 kwa ndege ya Shirika la ndege la (Tanzania Air Tanzania)
ambapo amesema Burundi imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa
za kifo cha Hayati Benjamin William Mkapa na hivyo kutokana na urafiki
wa kindugu baina ya Tanzania na Burundi amekuja nchini kuwakilisha
wananchi Waburundi kuomboleza na Watanzania kifo cha Mkapa.
Katika
msafara wake Waziri Mkuu huyo ameambatana pia na Spika wa Baraza la
Seneti la Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo ambaye kwa upande wake amesema
kifo kimeyapokonya Maisha ya Hayati Benjamin William Mkapa ambaye bado
alikuwa akihitajika kwa kiasi kikubwa hususani na Bara la Afrika
kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao katika usuluhishi na hivyo
Burundi imempoteza msuluhishi mkubwa.
Mbali
na Spika wa Baraza la Seneti la Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo,pia
Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni ameambatana na
Naibu katibu Mkuu wa chama kinachotawala nchini Burundi cha CNDD-FDD
Mhe. Joseph Ntakarutimana.
Akizungumza
mara baada ya kuwapokea viongozi hao Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema
wageni hao wamewasili jana Mkoani Kigoma wakitokea Burundi na baadae
kupanda ndege na kuwasili Dar es Salaam hii leo na kuongeza kuwa ujio wa
viongozi hao wa Burundi unaidhihirishia dunia mahusiano mema nay a
kindugu yaliyopo kati ya Tanzania na Burundi bila ya kujali nyakati za
shida,kuomboleza ama raha.
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kutoa
taarifa za kuwasili kwa viongozi wa Mataifa mbalimbali katika maziko ya
kitaifa ya Hayati Benjamin William Mkapa kwa kadri zitakavyopokelewa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Jenerali Alain Guillaume Bunyoni
akishuka kwenye mdege ya Shirika la Ndege la Tanzania mara baada ya
kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria
maziko ya kitaifa ya Hayati Benjamini William Mkapa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Burundi Mhe. Jenerali Alain Guillaume Bunyoni mara baada ya kuwasili nchini kuhudhuria maziko ya kitaifa ya Hayati Benjamini William Mkapa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Waziri Mkuu wa Burundi Mhe. Jenerali Alain Guillaume Bunyoni mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria maziko ya kitaifa ya Hayati Benjamini William Mkapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...