Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam
ya Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi (aliyevaa Barakoa)
akimwonesha Mkuu wa Chuo michoro na ripoti ya maendeleo ya ukarabati na
Ujenzi wa Madarasa Tegeta.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji
Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta akiwa kwenye picha ya pamoja na
Menejimenti na wafanyakazi wa Kampasi ya Dar es Salaam alipotembelea
Kampasi hivyo

Baadhi wa wanafunzi wa Masomo ya
Umahiri Kampasi ya Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo
Kikuu Mzumbe Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta alipotembelea Kampasi
hiyo

Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam
ya Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akiwa ameambatana na Mkuu wa
Chuo na Menejimenti ya Chuo hicho walipowasili kukagua miundombinu ya
ujenzi Tawi la Chuo Kikuu Mzumbe

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji
Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta akiwa na viongozi wa juu wa chuo hicho,
akiangalia kwa makini ubora wa samani zilizofungwa kwenye moja ya
madarasa yatakayotumika Tawi la Tegeta.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji
Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta (Katikati wa kwanza kushoto) akiwa amekaa
kwenye Viti katika moja ya madarasa yaliyokamilika Tegeta Kampasi ya
Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka na
wa mwisho kushoto ni Prof. Ganka Nyamsogoro Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Taaluma. Kulia wa kwanza ni Prof. Honest Ngowi Mkuu wa Kampasi ya Dar
(mwenye shati jeupe) akifuatiwa na Prof. Ernest Kihanga Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo Fedha na Utawala.
………………………………………………….
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta amefanya ziara ya kikazi Kampasi ya Dar es Salaam na kupongeza jitihada kubwa zilizofanyika za kupandisha hadhi Kampasi hiyo kuwa Ndaki “Campus College”.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta amefanya ziara ya kikazi Kampasi ya Dar es Salaam na kupongeza jitihada kubwa zilizofanyika za kupandisha hadhi Kampasi hiyo kuwa Ndaki “Campus College”.
Katika ziara hivyo Mhe.
Samatta aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza CPA. Pius Maneno,
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Lughano Kusiluka na wajumbe wa
Menejimenti; na kuzungumza na Wafanyakazi, Wanafunzi na kukagua
maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa miundombonu Tegeta, eneo ambalo
limeandaliwa kwa ajili ya masomo ya Shahada za Kwanza mwaka wa masomo
2020/2021.
Akizungumza mara baada ya
kukagua miundombinu ya Chuo hicho, Mhe. Samatta ameupongeza uongozi kwa
jitihada na mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi Tegeta,
akilinganisha na taswira aliyoiacha wakati alipofanya ziara yake ya
mwisho mwaka jana 2019.
“Nimefarijika sana kuona
mabadiliko haya makubwa kwakweli sikutegemea. Ila nina imani kubwa kituo
hiki kitafungua fursa nyingi na kuongeza idadi ya wananchi wanaotaka
kujiendeleza na Elimu ya Juu, kwakuwa hapo awali walilazimika kwenda
kufuata masomo ya shahada za awali kwenye Kampasi zetu Morogoro au
Mbeya…” akisisitiza
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka, amesema tayari Chuo
kimeshapata idhini ya kuanzisha kozi za awali Tegeta kutoka Tume ya Vyuo
Vikuu(TCU) na kwamba wanaendelea na hatua za mwisho za maandalizi ya
miundombinu kwaajili ya kupokea wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo na
kwa kuanza wataanza na kozi mbili za awali ambazo ni Shahada ya Utawala
wa Umma (Bachelor of Public Administration -BPA) na Shahada ya Uhasibu
na Fedha- Sekta ya Biashara (Bachelor of Accountancy and Finance-
Business Sector (BAF-BS).
Ziara ya Mkuu wa Chuo Jaji
Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea kila
mwaka wa kutembelea Kampasi zote zilizopo chini ya Chuo hicho, kukagua
shughuli na miradi ya maendeleo, kuzungumza na Wafanyakazi na
Wanafunzi, pamoja na kujibu hoja mbalimbali. Hii ni ziara yake ya
mwisho kufuatia muda wake wa uongozi kufikia tamati ambapo tarehe 13
Januari 2021 atakuwa ametimiza miaka 11 ya uongozi wake tangu
alipoteuliwa mwaka 2009 na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete kushika wadhifa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...