
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw. Gerald Kusaya akiongea na waandishi wa wa habari mjini Katavi ambapo
alisema amerIdhishwa na kasi ya mkandarasi anayejenga vihenge vya
kisasa na ghala chini Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda
ya Katavi.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kushoto) akizungumza na
wakandarasi wa kampuni ya M/S Unia Araj Spoo ya Poland wanaojenga
vihenge sita vya kisasa na ghal moja NFRA kanda ya Mpanda jana
alipotembelea kukagua mradi huo utakaokamilika Novemba 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya (kulia) akiongea na watumishi wa NFRA ofisi ya Mpanda
jana mara baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vihenge na
maghala.Amewataka watumishi hao kujituma na kufanya kazi kwa weledi ili
nafaka iliyohifadhiwa kwenye maghala idumu kwa muda mrefu na kuendelea
kuwa bora.
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald
Kusaya akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji mkoa wa Katavi jana alipowatembelea kukagua utendaji kazi
wao changamoto wanazopitia ili kuzitafutia ufumbuzi.
Mwonekano wa picha za vihenge vya kisasa vinavyojengwa mjini Mpanda ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka chini ya NFRA .
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Mhe. Juma Homera (kushoto) na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa
Katavi Bw. Abdalla Malela jana wakati wa ziara ya kikazi mkoani Katavi.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (wa pili toka kulia) akikagua ghala linalojengwa kwenye kituo cha NFRA kanda ya Mpanda. Ghala hilo litakiuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka litakapokamika Novemba 2020.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...