Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2021. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Amour Hamil Bakari (kushoto). Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2021. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2021. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Saalam. Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo Mhe.Innocent Bashungwa. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Amour Hamil Bakari (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo alipokua akizungumza katika  kikao cha Maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2021. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Amour Hamil Bakari (kushoto),pamoja na mwanariadha  mashuhuri Bw. Seleman Nyambui  baada ya  kikao cha Maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2021. Kikao hicho kilichorikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Olimpiki Tanzania pamoja na Mashirikisho ya Riadha na Ngumi kilifanyika Desemba 22, 2020 Jijini Dar es Salam.

**************************************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesisitiza kuwa Michezo itaendelea kuwa nyenzo katika kudumisha Muungano.

Mhe. Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Desemba 22, 2020, Jijini Dar es Salaam katika Kikao cha Maandalizi ya kushiriki Michezo ya Olimpiki Tokyo mwaka 2021.

Akiendelea kuzungumza katika Kikao hicho kilichoshirikisha Baraza la Michezo la Taifa, Baraza la Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Kamati ya Maandalizi ya Olimpiki, Chama cha Riadha pamoja na Shirikisho la ngumi alisema kikao hicho kinalenga kujadili namna Taifa hili litakavyoshiriki Michezo hiyo.

“Naendelea kusisitiza suala la Utawala Bora kwa Vyama na Mashirikisho yote ya Michezo, pia hakikisheni mnasaidia ustawi wa timu zetu za Taifa,”alisema, Mhe.Bashungwa.

Aidha, Mhe.Bashungwa aliagiza kuwa Maazimio yote ya kikao hicho yafanyiwe kazi, ikiwemo maandalizi ya kutosha ya Michezo ya Kimataifa pamoja na uwezo wanamichezo wanaoshiriki mashindano hayo. 

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega amevitaka Vyama na Mashirikisho ya Michezo kuwa na vipaumbele katika michezo, ambapo amesisitiza kuwa lazima nchi kuwa na michezo ya vipaumbele ambayo itafanya vizuri ndani na nje ya nchi.

“Sisi wasimamizi wa Sekta ya Michezo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tutasimamia maono ya Marais wetu katika kukuza na kuendeleleza Sekta hizi,” alisema, Mhe.Ulega.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kulifikisha Taifa hili linapostahili katika sekta ya michezo, huku akisistiza kuwa suala la kuwa na chanzo cha kuaminika katika kuendesha michezo Serikali inaendelea kulisimamia.

Vilevile, Mwanariadha wa zamani Bw.Selemani Nyambui ameipongeza Serikali kwa dhamira yake ya kukuza michezo ambapo amesema kuwa sekta hiyo ni muhimu katika ustawi wa vijana wenye vipaji na ari ya kuisaidia nchi kupitia michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...