Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiwahutubuha waalikwa wa hfla ya makabidhiano ya kompyuta zilizotolewa na Benki ya CRDB leo katika katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma leo tarehe 31 Desemba, 2020.
1. Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Dkt. Benson Ndiege akitoa neon katika hafla hiyo ya makabidhiano ya kompyuta 100 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwenda kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika.
1. Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na Watumishi wa Benki ya CRDB wakifuatilia hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Tume Jijini Dodoma.

1. Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akimkabidhi Mrajis Mkuu wa Vyama vya
Ushirika Tanzania Bara Dkt. Benson Ndiege kompyuta alipokea kutoka kwa Benki ya
CRDB Jijini Dodoma leo.
1. Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiwa pamoja na Mrajis Mkuu wa Vyama
vya Ushirika Tanzania Bara Dkt. Benson Ndiege na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Benki ya CRDB nchini Bwana Prosper Nambaya pamoja na Watumishi wa Benki ya
CRDB pamoja na Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika mara baada ya hafla
ya makabidhiano ya kompyuta kutoka Benki hiyo.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Bwana Gerald Kusaya amesema majukumu makubwa ya Tume ya Maendeleo ya
Ushirika ambayo ni udhibiti, usimamizi pamoja na uhamasishaji wa Vyama vya
Ushirika hayawezi kutekelezwa ipasavyo bila ya kuwa na mifumo thabiti
inayojengwa kwa vitendea kazi zikiwemo kompyuta na vyombo vya usafiri.
Katibu Mkuu Kusaya ameyasema
hayo leo tarehe 31 Desemba, 2020 wakati
akipokea kompyuta 100 za mezani (Desktop) kutoka kwa Benki ya CRDB; Kompyuta
hizo zimetolewa na Benki hiyo kama sehemu ya kuunga mkono utendaji kazi wa Tume
ya Maendeleo ya Ushirika hususan eneo la usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara
wa Vyama vya Ushirika.
Katibu Mkuu Gerald Kusaya
amepokea kompyuta hizo 100 zenye thamani ya shilingi milioni 150 Jijini Dodoma
katika ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika kutoka kwa Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB nchini Bwana Prosper Nambaya.
Katibu Mkuu Kusaya amesema kompyuta
hizo 100 zitaongeza kasi na uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuongeza utoaji wa huduma
kwa Wanaushirika kote nchini pamoja na kuongeza ufanisi katika shughuli zote za
usimamizi wa Vyama vya Ushirika.
“Kompyuta hizi
zinazokabidhiwa leo kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika zitaongeza kasi ya
uwajibikaji kwa Watumishi wa Tume katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku
katika kushughulikia maombi ya leseni na utoaji wake kwa Vyama vya Ushirika wa
Akiba na Mikopo (SACCOS) kote nchini”.
“Itakumbukwa kuwa Sheria ya
Huduma Ndogo za Fedha Na.10 ya Mwaka 2018 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2019,
zinaelekeza kila Mtoa huduma ndogo za fedha nchini zikiwemo SACCOS kutakiwa
kuomba leseni kwa mujibu wa sheria hiyo. Hivyo, kutolewa kwa kompyuta hizi
kutasaidia Ofisi kusimamia zoezi la utoaji wa leseni (ambazo zimekuwa zikiombwa
na kutolewa kwa njia ya mtandao – SACCOS Online Application System).”
“Kuongeza ufanisi na kasi
katika utendaji kazi wa shughuli za kila siku kwa Watumishi wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika, ili kuvisimamia kikamiifu Vyama vya Ushirika kwa njia za
mifumo ya kiusimamizi”
“Kuongeza ufanisi katika
upatikanaji, utunzaji na utoaji wa taarifa na takwimu mbalimbali za Vyama vya
Ushirika kama vile Idadi ya Vyama, Wanachama, Hisa, Mtaji uzungukao, Ukaguzi,
Usajili, Kesi na Migogoro, Uwekezaji, Masoko, Madeni n.k.” Amekaririwa Katibu
Mkuu Kusaya.
Naye Mrajis wa Ushirika
nchini Dkt. Benson Ndiege amesema msaada huo wa kompyuta kutoka kwa Benki ya
CRDB utaongeza ufanisi kutokana na Watumishi kadhaa wa Tume hiyo kukabiliwa na
upungufu wa vitendea kazi kama kopyuta pamoja na usafiri.
“Tume ya Maendeleo ya
Ushirika kazi zetu zilikuwa haziendi vizuri kutoakana na baadhi ya Wataalam
kukosa vitendea kazi zikiwemo kopyuta; Kuna Maafisa hawana kompyuta kabisa na
hivyo kufanya kazi, wanawasubiri wengine wawe wametoka au wawaombe pale amabapo
hazitumiki. Kutolewa wa kompyuta hizi kutaongeza tija kwenye majukumu yetu ya
kila siku yakiwemo ukusanyaji wa takwimu, kuratibu mafunzo, kufanya tafiti,
kuratibu uhamasishaji na nyingine.”
“Naomba kuwahakikishia Benki
ya CRDB kuwa tutaendelea kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo ya
Wananchi wetu. Hasa pape Benki inayofanya biashara au kuwahudumia Wakulima kwa
njia ya kutoa mikopo na ushauri wa kifedha.”
“Tume kupitia Maafisa wake na
Vyama vya Ushirika watawasaidia kutoa taarifa za kutosha za Wakulima wanaotaka
kukopeshwa na Benki hii.” Amekaririwa Mrajis Mkuu Dkt. Benson Ndiege.
Naye Mkurugenzi wa Wateja
Wakubwa CRDB Bwana Prosper Nabaya akiongea kwa naiba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Benki hiyo amesema Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo
kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuongeza kuwa hadi sasa Benki hiyo
imewakopesha Wakulima walio kwenye Vyama vya Ushirika zaidi ya bilioni 650.
Bwana Prosper Nambaya
ameongeza kuwa CRDB imekuwa ndiyo Benki pekee inayofanya kazi za Wakulima wengi
nchi kuliko Benki yoyote.
“Katika mwaka wa fedha wa
2019/20 Benki ya CRDB imetoa jumla ya mikopo ya kilimo ya shilingi bilioni 650
sawa na asilimia 40% ya mikipo yote ya kilimo nchini Tanzania. Kati ya mikopo hiyo bilioni 495 imeelekezwa
kwenye mazao makuu ya kimkakati hivyo kumsaidia zaidi ya AMCOS 472 kupata
mikopo kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo (mikopo ya
pembejeo, maghala, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao, mikopo kwa ajili ya
miradi ya ufugaji, uwekezaji kwenye misitu na mazao yake pia uwekezaji kwenye
uvuvi.” Amekaririwa Bwana Nambaya.
Bwana Nambaya amesema Benki
ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kufufua Ushirika kwa kuongeza mitaji ili
kuhuisha na kuujenga Ushirika imara (TACOBA & KCBL).
“Benki ya CRDB inatoa mchango
mkubwa kwa wana ushirika kupitia mafunzo na misaada ya vifaa muhimu vya
kufanyia kazi kama vile kompyuta.”
“Tunatoa wito wa
kuvikaribisha Vyama vyote vya Ushirika nchini kujiunga na Benki ya CRDB ili
viweze kujikwamua kiuchumi na kupata mazingira wezeshi kwenye sekta zote za
kiuchumi.” Amekaririwa Mkurugenzi Nambaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...