Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WADAU wa mazingira na hasa ambao wamejikita katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na mipango bora ya matumizi ya ardhi wamesisitiza umuhimu wa jamii kuendelea kupatiwa elimu itakayoweza kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuzingatia matumizi bora ya ardhii.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kujadiliana na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na matumizi bora ya ardhi wamesema kuna changamoto nyingi zinatokea na sababu yake kubwa inatokana na mabadiliko ya tabianchi.

Meneja Mradi wa Shirika la African Climate Justice Alliance(PACJA) Project Collin Oduor kutoka Kenya amesema awali walifanya utafiti kupitia FORUMCC na utafiti ulihusu matumizi ya ardhi yanavyohusishwa na mabadiliko ya tabianchi.

"Kama tunavyojua vile tunavyotumia ardhi ndivyo tunavyoendeleza makali au kuyapunguza mabadiliko ya tabianchi.Tanzania kupitia utafiti uliofanyika waligundua matumizi ya ardhi yanachangia katika mabadiliko ya tabianchi kwa kiwango fulani.

"Kwa kawaida Afrika au nchi zinazoendelea kilimo, misitu inachangia sekta nyingine katika mabadiliko ya tabianchi.Hivyo kukutana kwetu leo ni kuhakikisha tunahamasisha mashirika ya kijamii wameenda kule ambako wanafanya kazi.

"Wanafahamu kupanga na kutumia ardhi yako vizuru kunaweza kusaidia kupunguza makali ya mabadiliko ya tabianchi.Mbadala wa matumizi ya ardhi baada ya mabadiliko ya tabianchi kutokea,"amesema.

Amefafanua kutokana kasi ya maendeleo inayoendelea kufanyika kumekuwepo na matumizi makubwa ya ardhi na miti imendelea kukatwa, ardhi yenye rotuba inaendelea kutoweka, hivyo ni muhimu kuhakikisha jamii inaendelea kutunza mazingira.

"Nimekuja jijini Dar es Salaam juzi nimekuta joto liko nyuzi joto 31 wakati kule Kenya joto liko chini ya nyuzijoto 20, najua Dar iko karibu na bahari lakini kuna uwezekano kubwa tukipanda miti kutasadia kurejesha hali ya uhifadhi ili kurejesha joto chini,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Sauti ya Haki Tanzania, Wakili Letitia Petro amesema shirika hilo kimsingi limejikita kulinda na kutetea haki za binadamu na hasa wanawake na watoto.

"Kitu kikubwa ambacho tumekuwa tukikifanya ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria hasa kwa akina mama ambao wanakuwa na migogoro ya ardhi.Makao yetu makuu yako wilayani Rungwe lakini na nchi nzima kwasababu tunawanawachama mikoa mbalimbali.

"Sasa leo katika mafunzo haya ambayo kimsingi yanahusu mabadiliko ya tabianchi pamoja na matumizi bora ya ardhi yamekuja wakati muafaka kwasababu Taifa letu na dunia nzima inayo changamoto ya mabadiliko ya tabianchi lakini pia kwenye suala la matumizi bora ya ardhi imekuwa ni changamoto kwa kila nchi na sio tanzania tu.

"Tumefika wakati hata ukiangalia Wilaya ya Rungwe zamani tunaambiwa walikuwa wanaita London ya Afrika kutokana na baridi ya kutosha,hakukua na magonjwa, mito inatitirika, kuna misitu , kila sehemu uliyokuwa ikikanyaga wanasema ilikuwa ya kijani,"amesema.

Amefafanua lakini ukiangalia wakati huu wanapata mpaka joto kwa mfano kipindi hiki kuna joto la kutosha wilayani Rungwe kitu ambacho kinaonesha kuna mabadiliko yametokea, moja wananchi wengi wamejenga na wanalima kwenye vyanzo vya maji.

"Hata suala la miti mfano mtu akikata miti mara nyingi hana mpango wa kurejesha ile miti ambayo itasaidida mvua kuendelea kunyesha , kwa hiyo kazi za kibanadmu ambazo zinafanya zimekuwa chanzo kimojawapo cha kuharibu mazingira na uoto wa asili.

"Japo niseme kwa upande wa Serikali angalau imeweza kujitahidi inaweka maonyo kama watu wasijenge katika vyanzo vya maji, watu wasikate miti bila vibali, lakini ukiangalia hizo jitihada bado hazijajitosheleza ,ukiangalia hii elimu ambayo tumepatiwa leo tunaona kabisa tunahitaji kuijenga hata kwa wananchi wa kawaida wajue umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.

"Wajue umuhimu kutunza misitu, wafahamu umuhimu wa wao kuwa mabalozi wa kila mwananchi aliyekuwa kwenye eneo kwamba wasiharibu mazingira yaliyopo kwani maisha ya binadamu yoyote yanategemea mazingira,"amesema.

Amesisitiza mazingira yakishakuwa yameharibika kutakuwa na hewa chafu, mafuriko , ukame na kila kitu katika maisha yatabadilika, hivyo ni wajibu wa Serikali, wadau kama taasisi zao ambazo  zisizokuwa na kiserikali na taasisi za kiserikali kuhakikisha kila mwananchi atashirikishwa kulinda mazingira na kuzingatia matumizi bora ya ardhi.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi , Usimamizi pamoja na  Uratibu kutoka Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Joseph John amesema ni ukweli usiopinga kuna mabadiliko ya tabianchi yanaendelea na yana madhara mengi.

"Nchi yetu ina mikakati na imeingia kwenye makubaliano kwa ajili ya kuhakikisha inasaidia au inachangia katika kuzuia ongezeko la madhara ya mabadiliko ya tabianchi,pia inapambana kuzuia isiwepo lakini kwa wakati huo huo Serikali iliunda chombo kikuu kinachosimamia uratibu wa maandalizi ya matumizi ya mipango ya ardhi nchini, chombo hicho kinaitwa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

"Chombo hiki kina kazi nyingi lakini mojawapo ya kazi ni kuratibu wadau mbalimbali wenye nia ya kusaidia kuwezesha upangaji wa matumizi bora ya ardhi, sasa ukija kwenye suala la athari ya mabadiliko ya tabianchi tunashuhudia kuna ongezeko kubwa sana la joto nchini.

"Pia kuna mabadiliko sana ya hali ya hewa, kuna ukame unaongezeka sana, mvua zisizokuwa na utabiri, kuna muda mwingine hata misimu ya mvua kama itunachanganya vile, kuna vitu vingi vinabadilika na kubadilika huko kuna madhara katika maisha ya binadamu,"amesema.

Mkurugenzi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi , Usimamizi na  Uratibu kutoka Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Joseph John akisisitiza jambo wakati akizungumzia namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na wadau katika kupanga matumizi bora ya ardhi.

Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Muna akifurahia jambo wakati wa mkutano huo uliohusisha wadau kutoka mashirika mbalimbali kujadili na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Sauti ya Haki Tanzania, Wakili Letitia Petro akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kuzingatia matumizi bora ya ardhi.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kuweka mipango ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na mipango bora ya matumizi ya ardhi wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na FORUMCC na Shirika la African Climate Justice Alliance(PACJA) ambao wadau kutoka mashirika mbalimbali wameshiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...