Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WADAU kutoka mashirika na Asasi za kiraia ambazo zimejikita katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi wakiongozwa na FORUMCC wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha na kuweka mikakati kuhakikisha wanaendelea kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza leo wakati wa kikao cha wadau hao kutoka mikoa yote nchini, Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Muna amesema wanafanya kazi katika ngazi zote na inauwakilishi wa shughuli mbalimbali za uhamasishaji katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya kitaifa.

Amesisitiza lengo la kukutana kwao ni kuongeza chachu na hamasa ya wadau na wanachama wao kuongeza kasi ya uhamasishaji namna ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchia, hivyo wameandaa mkutano huo ambao umeleta wanachama wake kutoka Tanzania nzima.

"Tumekutana katika mkutano huu ili tuweze kukaa pamoja na kupanga mikakati kuhakikiha kwamba sasa hivi tunaongeza jitihada za ushirikishaji katika ngazi zote husasani kule kwenye wananchi, viongozi wa serikali za mitaa na kuona namna ambavyo watu wanakuwa na uelewa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

"Ikiwa na hatua ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchi ili majanga yanapokuwa dhahiri kabisa yasiweze kuleta athari kubwa kiuchumi katika masuala ya uhakika wa chakula na kipato cha mtu mmoja mmoja lakini masuala ya afya kwani athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi yanaathiri afya.

"Na mambo ambayo ni muhimu jamii yetu kuyajua , kwa hiyo leo tutapanga mikakati , tutakumbushana , kuongeza hamasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na leo hii tumekutana wadau wengi.Hii imekuwa ni muhimu sana kuwa na wadau wengi katika kukabiliana na athari hizo, kuwa na uelewa mkubwa waanchi, viongozi , watendaji na wafanya maamuzi na wanasiasa ili kulipa kipaumbele mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi,"amesema Muna.

Aidha amesema joto ambalo lipo hivi sasa ni sehemu ya athari za mabadiliko ya tabianchi na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetoa taarifa za kwamba baadhi ya mikoa itakuwa na joto kali sana.Pia takwimu zinaonesha hali inazidi kuwa mbaya na ngumu kutokana na kuendelea kwa athari hizo.

"Uthibitisho wa athari za mabadiliko ya tabianchi ni taarifa ambayo imetolewa ya kwamba joto litaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya mikoa lakini pia inaathari kwa uchumi mpana wa nchi, kwa uchumi wetu unategemea usalama wa hali ya hewa,joto linapoongezeka lazima tujue maana yake nini kwenye maji, maana yake nini kwa kilimo, maana yake nini kwa wafanyakazi na maeneo mengine mengi,"amesema.

Hivyo amesema kwa hiyo katika mkutano wao wa leo watangaalia jinsi ya kuchukua hatua lakini kuwa na mikakati ya kuhamasisha viongozi wakiwamo watoa mamuzi kuweka mikakati ya kuhimili athari ambazo zitatokana na kupanda kwa joto.

"Tunafaham athari za mabadiliko ya tabianchi hazizuiliki ila tunatakiwa kutafuta namna ya kuishi katika jilo joto ambalo nalo ni matokeo ya athari za mabadiliko ya tabianchi.Hakuna teknolojia ya kuondoa hali ya joto , lakini sisi kama Watanzania tutawezaje kuboresha mundombinu, teknolojia na uelewa kwa wananchi ili joto linapoongezeka kusiwe na athari kubwa katika maisha yetu ya kila siku pamoja na vyanzo vyetu vya kiuchumi,"amesema Muna.

Kwa upande wa wadau walioshiriki mkutano huo wameeleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga imara katika kuhakikisha jamii ya watanzania inaendelea kupata uelewa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kushirikiana na wadau wengine ambao wamejikita katika kukabiliana athari hizo.

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa FORUMCC Jackson Muro amesema katika mkutano huo wa wadau pamoja na mambo mengine walikuwa wanajadiliana kuhusu mtazamo wa watu, hisia za watu katika kufahamu mabadiliko ya tabianchi, kwanza waelewe hali ya mabadiliko ya tabianchi ipo na itaendelea kuwepo lakini wanafanyaje ili wasife , wanafanya ili watu wasife.

"Tufanyeje ili mifugo isife, tufanyeje ili kilimo kisimame katika mabadiliko hayo.Hata hivyo tumefanikiwa kwasababu tumeona watu waliokuwa wanategemea mfumo mmoja wa uzalishaji kama wafugaji waliokuwa wanategemea mifugo peke yake leo kuna wafugaji wanalima,wako ambao wamejiingiza kwenye biashara za madini, wako waliojiingiza kwenye biashara ndogondogo, wanafanya ili kujiimarisha kiuchumi wakati mabadiliko ya tabianchi yanaendelea.

"Leo baada ya hapa utaona kuna vikundi vya wanawake wajasiriamali ambao yankini wengine walikuwa wanatagemea huku Dar es Salaam kuchukua samaki lakini mabadiliko ya tabianchi yanamadhara , katika samaki na mifugo.

Amefafanua hivyo samaki nao wanakuwa juu na kumfanya mjasiriamali kushindwa kundelea na biashara ya samaki, kwa hiyo wanalazimika kufanya kitu mbadala kama kushona nguo au kutengeneza mkaa mbadala na hayo wanayaona ni mafanikio ambayo FORUMCC imeyapata kutokana na kuwajengea uelewa wananchi.


Makamu Mwenyekiti wa FORUMCC Jackson Muro akizungumzia umuhimu wa mkutano uliowakutanisha wadau hao katika kujadili masuala mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Muna akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliwakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali yasiyoyakiserikali ambayo yamejikita katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Wadau wa mazingira wakiendelea na kazi ya kujaza maelezo kwenye karatasi baada ya kutakiwa kufanya hivyo kutokana na mijadala iliyokuwa ikiendelea wakati wa mkutano huo.

Sehemu ya wadau wakiendelea kufuatilia kwa makini mijadala iliyokuwa ikiendelea wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya wadau hao wakimsikiliza Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Muna(hayupo pichani) wakati akiwajengea uwezo wa namna na kufanya shughuli zao katika kuhakikisha wanaendelea katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mmoja wa wadau kutoka Zanzibar akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo uliwakutanisha wadau wa masuala ya mazingira na hasa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi waliokuwa chini ya mwamvuli wa FORUMCC .

Sehemu ya wadau wa mazingira walioshiriki mkutano huo wakiendelea kuandika mambo muhimu yaliyokuwa yakijadiliwa.Pia walitaka kuandika kwenye karatasi kila mtu kwa maono yake kuhusu namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Baadhi ya wadau kutoka mashirika mbalimbali yanayokabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi wakiandika maelezo wakati wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Muna akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili na kuweka mikakati ya kuendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliohusisha wadau kutoka mashirika na asasi mbalimbali mikoa yote nchini ambao wamejikita katika mabadiliko yatabianchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...