MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafikisha mahakamani wa tu wawili kwa makosa ya wizi na utakatishaji fedha zaidi ya Sh. milioni 168.

Washtakiwa hao ni Fred Manjiu mkazi wa Kimara Temboni na Arbogast Christian mkazi wa Mkuranga walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu ambapo upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu akisaidiana na Wakili wa Serikali Kija Luzungana.

Akiwasomea mashtaka Wakili Marandu alidai katika shtaka la kwanza washtakiwa hao pamoja na wengine ambao hawajakamatwa waliandaa na kuongoza genge la uhalifu kwa kukusudia na kutenda kosa la wizi wa vifaa mbalimbali vya umeme vyenye thamani ya Sh. 168,188,543.52 mali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kosa wanalodaiwa kulitenda kati ya Jan, 2017 na Novemba 14, 2020 katika eneo la Kimara Temboni.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao pamoja na wengine ambao hawajamatwa, wanakabiliwa na kosa la wizi ambapo wakili Marandu alidai kati ya January, 2017 na Novemba 14, 2020 huko Kimara Temboni waliiba vifaa hivyo mali ya Tanesco.

Aliendelea kudai katika shtaka la tatu la utakatishaji fedha washtakiwa hao pamoja na wengine ambao hawajakamatwa katibya Januari, 2017 na Novemba 14, 2020 kwa pamoja walijihusisha na miamala ya fedha Sh 168,188,542.52 huku wakijua ni mazalia ya makosa tangulizi ya wizi na kuongoza genge la uhalifu.

Katika shtaka la mwisho washtakiwa hao pamoja na wengine ambao hawajakamatwa wanadaiwa kati ya Januari, 2017 na Novemba 14, 2020 waliisababishia Tanesco hasara ya Sh. 168,188,542.52.

Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili Marandu alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 24, 2020 na washtakiwa walipelekwa mahabusu kwa kuwa moja ya mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...