*******************************
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
Des 11
MBUNGE wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewahakikishia wananchi wa Kata ya Pera na
Chalinze kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za migogoro ya Ardhi
katika Halmashauri hiyo .
Akizungumza na
wananchi wa Kata ya Pera ,aliwahakikishia wananchi kuwa wamejipanga
vizuri kumaliza kero za mipaka hasa ile isiyokwisha kati ya Kitongoji
cha Pingo na Chamakweza ambao umedumu kwa takribani miongo Miwili.
Awali akiwa katika
Kitongoji cha Pingo, Mbunge aliweza kufanya mkutano wa wazi na Wananchi
ambapo pia aliongozana na watalaam mbalimbali wa Idara pamoja na
viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Kata na Wilaya wakiwemo Wanasiasa.
Mbunge amewaahidi
Wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano huku akiwashukuru kwa
kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwemo kumpatia asilimia zaidi ya 94
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli.
Katika mkutano huo ambao Mbunge alipokea pia kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwemo migogoro ya mipaka,
Mgogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, Fursa za TASAF, mikopo ya Jamii , Afya na mengineyo.
Hata hivyo Mbunge
aliweza kutolea ufafanuzi baadhi ya kero za Wananchi ambazo zimeanza
kufanyiwa kazi na kuwakumbusha kuwa serikali haikuwa imelala ilikuwa
inafanya kazi, huku zingine akiahidi kuzichukua kwa ajili ya
kuzitafutia ufumbuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...