Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni Fred Manjiu (46) Fundi Umeme ambaye ni mkazi wa Kimara Temboni na Arobogast Christian (60) Mfanyabiashara ambaye ni mkazi wa Mkuranga B. Wakazi hao wamefikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu.
Awali, wakisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu Martenus Marandu akisaidiana na Wakili wa Serikali Kijja Elias alidai, Januari mwaka 2017 na Novemba 14, mwaka 2020 washtakiwa waliongoza genge la uhalifu na kuiba vifaa mbalimbali vya TANESCO.
Shtaka la pili, Wakili Marandu alidai, washtakiwa wanakabiliwa na kosa la wizi katika kesi ya Jinai namba 98/2020. Pia washtakiwa wanadaiwa , Januari 2017 na Novemba 14, mwaka 2020 wote kwa pamoja waliiba vifaa mbalimbali mali ya TANESCO vyenye thamani ya Sh.milioni 168,188,543.52.
Aidha amedai watuhumwa hao Januari 2017 na Novemba 14, 2020 katika eneo la Temboni jijini Dar es Salaam wote kwa pamoja walijihusisha na miamala ya fedha huku wakijuwa yalikuwa ni mazalia ya kosa tangulizi la wizi.
Wakati shtaka la nne, Wakili Marandu alidai, tarehe hiyo hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kuisababishia hasara mamlaka maalumu (TANESCO) ya Sh.milioni 168,188,543.52. Kabla ya kusomwa kwa mashtaka hayo, Hakimu Chaungu alisema, washtakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Hata hivyo Wakili upande wa mashtaka alidai upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.Hakimu Chaungu ameahirisha kesi na watuhumiwa walirudishwa rumande hadi Desemba 24 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...