WAKAZI wa Mbezi Juu jijini Dar es Salaam wakishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Asasi ya Gender Action Tanzania(GATA), Serikali na Ofisi ya Ustawi wa Jamii wamesema kuna kila sababu ya jamii kushiriki kwenye kukomesha ukatili wa kijinsia katika jamii.
Wamesema kwamba siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni siku ambazo zipo kimataifa, kikanda,kitaifa na kwa kifupi ni siku ambayo iko Kidunia na lengo lake kuu ni kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania (GATA) Neema Makando amefafanua kwa hapa Tanzania siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ilizunduliwa Novemba 25, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika Dk.Tulia Ackson huku kauli mbiu ikiwa inasema "Tupinge ukatili wa kijinsia , mabadiliko yanaanza na mimi"
"Kwa hiyo GATA kwa kushirikiana na ofisi ya Kata ya Mbezi Juu na Ofisa ustawi wa jamii tunapinga ukatili huu wa kijinsia , kwa kupinga matendo yote ya ukatili wa kijinsi, kwa hiyo tumeandaa jukwaa moja kwa lengo la kukumbusha matendo ya ukatili wa kijinsia ni yapi, yanafananaje ili kuweza kuyazuia na yanapotokea tufanye kitu gani.
"Kwa hiyo katika eneo letu hili la Mbezi Juu tumeamua kwa pamoja kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali hasa kwa kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli katika kutekeleza ule mpango kazi wa taifa wa kwamba ukatili wa kijinsi sasa ufike mwisho na sisi tunataka kuona ukatili wa kijinsia unakoma,"amesema Makando.
Kwa upande wake Mwanasheria na Muelimishaji masuala ya kijinsia Maria Mruma amefafanua aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia ambapo aliamua kuzungumzia ukatili wa kjinsia ambapo amesema ni ule ukatili wa kisaikolojia au wa kiakili ambao muda mwingi huwa unaanzia chini hasa tangu utotoni.
"Na ukitaka kujua huyu mtoto kwa mfano walimu mashuleni ambao wanawafundisha wanajua kabisa huyu mtoto nyumbani kwao hakujatulia, pengine analialia hovyo, muda mwingine analala kwasababu nyumbani muda wa kulala hana , baba amerudi nyumbani na akifika tu anaanza kugombana na mama.Mtoto hapati muda wa kulala, hawezi kusoma .Wapo watoto wengine nyumbani wanafanya kazi nyingi maana kuna ule ubaguzi mtoto wa kike akirudi anatakiwa kuosha viombo na watoto wa kiume wanaambiwa wakacheze.
"Tunayaona hayo, mengine ambayo tunayafanya kwa kuona ni utamaduni wetu, ni utaratibu wetu lakini hatujui ni matendo ya ukatili wa kijinsia, tunavyopinga mwingine anaona ni utaratibu wake nyumbani.Kuna mzazi mwingine mtoto wa kiume atasoma anavyotaka lakini mtoto wa kike alipoishia ndio hapo hapo,hivyo tunaomba jamii ibadilike na tunaamini tutabadilika taratibu,"amesema.
Ameongeza kuna ukatili wa kijinsia ambao huo ni wa kingono , ubakaji, watoto wengi wanaingiliwa kinyume na maumbile na kesi hizo ni nyingi."Mimi nimefanya kazi Mahakama ya Temeke, kesi za aina hiyo zimekuwa nyingi sana, watoto wanaharibika, watoto wanaharibiwa.
"Yaani ukifika mahakamani utabaini wanaofanyia vitendo hivyo watoto ni ndugu wa karibu kabisa.Anakuja nyumbani anamfanyia hivyo mtoto, kwa hiyo saa zingine unashindwa kutambua mtoto yuko salama sehemu gani, maana akienda shule itakuja kesi ameitwa na mtu barabarani, akiwa nyumbani kesi itakuja amefanyiwa na mjomba,"amesema.
Aidha amesema kuna changamoto ya utolewaji wa taarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia."Kwani taarifa nyingi hazitolewi za kupingana na haya mambo ya ukatili wa kijinsia, mwanamke anaogopa kuripoti kufanyiwa ukatili wa kijinsi maana anawaza baada ya hapo anakwenda wapi, anahisi atafukuzwa."
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Shina Mbezi Juu ameeleza zamani ilikuwa wanaume ndio wenye kufanya ukatili wa kijinsia lakini siku hizi umekuwa ukifanywa na wanawake."Mimi kama Mwenyekiti wa Shina iliniuma mwanamke amemfanyia mwanaume wake ukatili wa kijinsia."Na yule mwanaume matokeo yake akapata na ajali, kalazwa na mwanamke akawa anatamba wala hakwenda kumsaidia mumewe.Wanawake sasa tubadilike ,tumekuwa wakatili kuliko wanaume.
Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Antida Gosbert ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa wazazi na walezi kukaa na watoto kwa upendo mkubwa sana na vema wakawa wanawadadisi watoto ili kujua mambo gani ya ukatili wa kijinsia anayofanyiwa.
"Hatutakiwi kuwa wakali sana,tunatakiwa kuwa wakali lakini tusiwe wakali sana, hata shuleni mtoto ana haki ya kusikilizwa , inafikia sehemu mtoto anataka kukwambia kitu wewe mzazi unaanza kumfokea, muache mtoto apate haki ya kusikilizwa.
"Pengine amefanyiwa ukatili na unapomfokea anashindwa kukupa taarifa yoyote, kwa hiyo watoto tuwe tunawasikiliza sana, tuwe tunafuatilia wanachosema, mwisho wa siku unapokuja kwenye ofisi zetu za ustawi unakuta mtoto ameshaharibika , lakini hakupata haki ya msingi ya kusikilizwa au kupendwa".
Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania (GATA) Neema Makando akieleza muendelezo wa kilele cha siku 16 za kukomesha ukatili wa kijinsia,ambapo hapa Tanzania siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ilizunduliwa Novemba 25, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika Dk.Tulia Ackson huku kauli mbiu ikiwa inasema "Tupinge ukatili wa kijinsia , mabadiliko yanaanza na mimi"" Kwa hiyo GATA kwa kushirikiana na ofisi ya Kata ya Mbezi Juu na Ofisa ustawi wa jamii tunapinga ukatili huu wa kijinsia , kwa kupinga matendo yote ya ukatili wa kijinsi, kwa hiyo tumeandaa jukwaa moja kwa lengo la kukumbusha matendo ya ukatili wa kijinsia ni yapi, yanafananaje ili kuweza kuyazuia na yanapotokea tufanye kitu gani",alisema Makando.
Mwanasheria na Muelimishaji masuala ya kijinsia Maria Mruma akizungumza mbele ya wageni waalikwa waliofika kushiriki tamasha fupi la muendelezo wa kilele cha siku 16 za kukomesha ukatili wa kijinsia,ambapo hapa Tanzania siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ilizunduliwa Novemba 25, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika Dk.Tulia Ackson huku kauli mbiu ikiwa inasema "Tupinge ukatili wa kijinsia , mabadiliko yanaanza na mimi"
Ofisa Ustawi wa Jamii Antida Gosbert akieleza umuhimu wa wazazi na walezi kukaa na watoto kwa upendo mkubwa,na kuwa Wadadidi kwa mtoto/watoto ili kujua mambo gani ya ukatili wa kijinsia anayofanyiwa.Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...