Kamanda  wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akizungumza na madereva katika cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi Ubungo Ibrahim Samwix akizungumza na madereva kuhusiana na sheria za Usalama Barabarani wakati utoaji elimu katika kituo hicho jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni Joseph Bukombe akitoa maelezo kuhusiana kuthamini maisha ya abiria wakati wakisafiri
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akipata maelezo kutoka Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi (mwenye koti na gloves ) Ibrahim Samwix wakati oparesheni katika kituo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akipata maelezo kutoka kwa Afande Ibrahim Samwix wakati Ukaguzi wa Mabasi ya mikoani.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi Ubungo Ibrahim Samwix akiwa katika Ukaguzi wa basi.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi Ubungo Ibrahim Samwix akiwa chini kufanya Ukaguzi wa basi.
Madereva wa Mabasi wakipata elimu ya Usalama Barabarani.
Mkurugenzi wa Sheria  wa RSA Augustus Fungo akizungumza namna wanavyotoa elimu ya Usalama Barabarani kama mabalozi.
Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kutoa elimu kwa madereva na abiria katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam.
 


*Samwix kufuta leseni kwa makosa ya mara kwa mara 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema madereva wasiofuata sheria halitawavumilia pamoja na kuwepo kwa opereshani mara kwa mara

Oparesheni katika kituo cha Ubungo ilihusisha Mamlaka ya Usafiri Barabarani (LATRA) Mabalozi wa Usalama Barabani (RSA) pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kikiongozwa Kamanda wa Kikosi hicho Wilbroad Mutafungwa.

Oparesheni hiyo ilikwenda kwa Ukaguzi wa Mabasi, Kuangalia nauli zilizowekwa zinaendana na tiketi za kampuni za mabasi.

Akizungumza katika Oparesheni na utoaji wa elimu  Kamanda  wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa wakati alipokuwa katika katika oparesheni na utoaji wa elimu kwa madereva wa Mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa nchi iko katika amani hivyo asitokee mtu akasababisha watu wengine wasiwe na amani kwa kusababisha ajali zinazotokana uzembe.

Aidha amesema kuwa wataendelea na oparesheni kwa nchi nzima pamoja uimarishaji wa taa za barabarani kwa madereva wasiofuata sheria za usalama Barabarani.

Nae Mkuu wa kituo cha Ukaguzi wa Mabasi katika kituo Mabasi Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa dereva yeyote atakayefanya makosa yanayojirudia watanyang'anywa leseni zao.

Amesema kuwa  madereva wanatakiwa kufuata sheria za usalama pamoja na kuhakikisha mabasi  yao yamekaguliwa.

Samwix amesema  madereva hawana sababu ya kukimbia   kwani wanaharibu mfumo wa breki na kumaliza tairi za Mabasi na kusababisha hasara kwa wamiliki wa Mabasi 

Mkurugenzi wa Sheria wa Mabalozi wa Usalama Barabani (RSA) Augustus Fungo amesema kuwa madereva wanawajibu wa kuwalinda abiria kwani ajali zinagharimu maisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...