MAHAKAMA Kuu Mwanza imetupilia mbali yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wajibu maombi katika kesi ya Mapitio namba 2/2020 iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Msikiti wa Ijumaa dhidi ya Bodi ya Shule ya Thaqaafa kwenye mahakama hiyo.

Mapingamizi hayo yametupwa na Jaji A.Z. Mgeyekwa wa Mahakama Kuu anayesikiliza kesi hiyo ya maombi ya mapitio namba 2 ya 2020 yanatokana na rufaa namba 30/2020 iliyokatwa na Bodi ya Thaqaafa.

Kabla ya kutuyatupilia mbali mapingamizi hayo,Wakili wa wajibu maombi Wilbard Kilenzi,akiwasilisha mapingamizi dhidi ya waleta maombi akipinga kuwa Abdallah Amin Abdallah,hana Locus(sehemu)ya kuwa Katibu wa Bodi ya msikiti wa Ijumaa.

Pia kiapo chake kilichopo mahakamani kililetwa bila idhini ya mahakama hivyo hakina mashiko ya kisheria na kuiomba itupilie mbali maombi ya waleta maombi kwa gharama.

Hata hivyo, Wakili wa waleta maombi Godfrey Samson wa LZone Allied Advocate akisaidiwa na Msafiri Henga, waliiomba mahakama kuyatupa mapingamizi ya wajibu maombi kwa gharama sababu hayakutastahili kuletwa kwa misingi ya kisheria.

Jaji Mgeyekwa alikubaliana na hoja ya mawakili wa waleta maombi dhidi ya  Bodi ya Thaqaafa ambapo aliendelea kusikiliza na maombi ya mapitio ya rufaa namba 30/2020 yaliyofunguliwa na Bodi ya Msikiti wa Ijumaa kisha akahairisha kesi hiyo hadi Disemba 14, mwaka huu atakapotoa uamuzi.

Rufaa hiyo Bodi ya Thaqaafa ilifungua kesi namba 11/2019 kwenye Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana ikipinga kulipa kodi ya pango sh. milioni 58 kwa mujibu wa mkataba wa upangaji kwenye Zahanati ya Msikiti wa Ijumaa Machi, 2015, wakidai licha ya kuwa ni wapangaji hawastahili kulipa.

Mahakama hiyo chini ya Hakimu Gwaye Sumaye alitoa uamuzi ikiitaka bodi hiyo kuheshimu mkataba wa upangaji wa 2015 ambapo Bodi ya Msikiti ilikaza baada kushinda kesi.

Hata hivyo, Mei 30, 2020 Bodi ya Thaqaafa ilikata rufaa namba 30 ya 2020 kwenye Mahakama Kuu Mwanza,shauri ambalo liliendeshwa hadi Septemba 16,2020 na kutolewa hukumu dhidi ya Bodi ya Msikiti wa Ijumaa.

Aidha Bodi ya Msikiti wa Ijumaa baada ya hukumu hiyo ilifungua  maombi ya Marejeo (Riview) namba 2/2020 mahakamani hapo wakidai hawakuwahi kupata wito wa kufika mahamakani kujibu rufaa iliyoipa ushindi Bodi ya Thaqaafa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...