Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kipokelewa rasmi na watumishi wa ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma hii leo Disemba 10, 2020.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili ofisini hapo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidi taarifa ya Utekelezaji Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kupokelewa rasmi katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akieleza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidi taarifa ya Utekelezaji Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi wakati wa kikao hicho.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akikabidhi taarifa ya Utekelezaji kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa ameongozana na Naibu Mawaziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Patrobas Katambi na Mhe. Ummy Nderiananga (mstari wa nyuma) mara baada ya kupokelewa rasmi katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. James Kajugusi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ofisi yake pamoja na Naibu Mawaziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Patrobas Katambi (Kazi, Vijana na Ajira) (kushoto) na (kulia) Mhe. Ummy Nderiananga (Wenye Ulemavu) mara baada ya kuhitimisha kikao cha Menejimenti.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Chamwino jana Disemba 9, 2020 Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...