Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amezindua mradi wa Maji eneo la Mnadani,Kata ya Mbalawala ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake ya kumaliza changamoto ya Maji katika Kata ya Mbalawala.

Awali wananchi wa eneo hilo walikuwa wakitumia umbali mrefu kufuata maji katika mitaa mingine hali ambayo imekuwa ikisababisha kutumia muda mrefu barabarani.

Aidha Diwani wa Kata ya Mbalawala Mh. Charles Ngh'ambi amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia upatikanaji wa visima vinne kwenye kata hiyo na hivyo kusaidia kutatua changamoto kubwa ya Maji iliyokuwa inawakabili wananchi wa eneo husika.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi,**Mzee Ainea Kusalula **amemshukuru Mbunge Mavunde kwa utatuzi wa kero ya maji katika kata hiyo na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge.

Ora et Labora "Sala na Kazi"

De Populo servorum "Mtumishi wa watu"


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...