Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga(kulia) akifuatiwa na Diwani kata ya Milo Robert pamoja na ndugu wa mbunge huyo waliposhiriki ibada katika kanisa la Anglikana.
Waumini wa kanisa la Anglikana Luana wakiwa wametulia wakimsiliza mbunge wao Joseph Kamonga (hayupo pichani.)
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana na wanakwaya ya kanisa katoliki parokia ya Luana.
Mbunge jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akizungumza na waumini wa kanisa katoliki parokia ya Luana. (Hawapo pichani.)
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa ameshika bakuli la sadaka huku waumini wakipita kutoa sadaka.


MBUNGE wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, ameahidi mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa  kanisa katoliki parokia ya Luana pamoja na shilingi milioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya mziki katika kanisa la Anglikana lililopo kata ya milo.

Ahadi hizo amezitoa alipotembelea makanisa hayo na kufanya ibada ambapo katika kanisa katoliki alisema mifuko hiyo ya saruji itawasili kabla ya mwezi huu kumalizika na itawasilishwa kanisani hapo.

Pia aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuungana naye katika kuchangia ili kuweza kujenga nyumba ya Mungu iliyo bora.

"Waumini wote tinapaswa kujitoa katika kutimiza kazi ya bwana kwani ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi ya Mungu kwa moyo." alisema Kamonga.

Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya ununuzi wa vyombo hivyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Milo Robert Njavike amesema ili kuweza kupata vyombo hivyo inawapasa kugharamia Tsh. Milioni 20.

Alisema fedha hizo zitatosheleza kupata vifaa hivyo vya kisasa kabisa na kuwawezesha kuabudu na kufurahi katika nyumba ya bwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...