Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland akimpa fedha mmoja ya mwananchi kwa ajili kumsaidia katika shughuli zake za ujasiriamali wakati akiwa katika ziara katika jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland  akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TURIWASA Kurwa Masanja wakati alipofanya ziara katika ofisi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland akizungumza na wananchi wakati wa ziara katika jimbo hilo.



MBUNGE wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland ameendelea na ziara yake katika Jimbo la Mvomero kwa kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira (TURIWASA)  pamoja na Shirika la Umeme (TANESCO) katika  Wilaya ya Mvomero.

Akizungumza  na viongozi wa Taasisi hizo katika ziara hiyo Zeeland amesema kuwa katika upatikanaji wa huduma ya maji kutoka TURIWASA wananchi wanakumbana na kero kwa kupata maji majira  usiku pekee  lakini ankara za maji zimekuwa kubwa tofauti na na matumizi ya maji hayo  licha ya kutoka usiku wa manane.

Zeeland  amesema baadhi ya  malalamiko ya wananchi wanadai kuwa maeneo mengine yanakosa maji kwa kipindi kirefu hivyo amemuomba Mkurugenzi wa TURIWASA Kurwa Masanja kuyafanyia kazi malalamiko hayo .

Aidha mbunge wa Jimbo hilo ameomba ofisi ya TURIWASA kutoa ushirikiano na ofisi ya mbunge ili kurahisisha utendaji kazi ikiwa na lengo moja kuwahudumia wananchi.

Pia Mkurugenzi wa TURIWASA Kurwa Masanja amempongeza mbunge kwa kuwasilisha kero hizo kwake na kusema ni kiongozi anayestahili kuigwa kwa kuonyesha vitendo namna anavyojali wananchi na Taasisi zilizopo kwenye Jimbo lake.

Masanja amesema kuwa anaanza kuchukua hatua mbalimbali baada ya Mbunge kuripoti  ofisini hapo huku Mamlaka ikiwa na mkakati wa kuongeza mitambo mikubwa yenye uwezo wa kusafirisha maji mengi, kuangalia njia mbadala ya kero za ankara  za maji kuwa kubwa, kuweka ratiba nzuri ya mgawo wa maji pamoja na kuhakikisha watumishi ambao hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi mitano wanalipwa mwezi huu pesa zao zote kama ambavyo mbunge amelalamikiwa na baadhi ya watumishi kuwa maisha yao yamekuwa magumu kutokana nakutolipwa mishahara .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...