Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (aliyevaa tai), akikagua matofali ya Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi, zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo leo, lengo ikiwa ni kutatua makazi ya askari hao.Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akipita mbele ya nyumba za askari polisi(zinazoonekana pichani) zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba ambazo zilijengwa na fedha zilizotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ikiwa ni mkakati maalumu wa kutatua changamoto za makazi ya askari nchini.Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akiteta jambo na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan(kulia)leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi, zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan (wapili kushoto),akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi,leo zilizopo eneo la Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...