RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA)
Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 16
ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Dk. Ali
Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 30-12-2020.(Picha na
Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametawazwa kuwa Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Ndg. Mwita Mgeni Mwita na (kulia
kwa Rais) Makamu Mkuu wa Chuo Dkt.Zakia Mohamed Abubakar, hafla hiyo
imefanyika wakati wa Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi
wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja
leo30/12/2020.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimtunuku Shahada ya
Heshima ya Udaktari wa Falsafa Katika Sayansi za Tiba Rais Mstaaf wa
Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Mahafali ya 16
ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliofanyika katika ukumbi
wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu leo 30-12-2020.(Picha na Ikulu)
WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya
Sayansi ya Kemia wakitunukiwa Shahada ya Uzamili na Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo
pichani) wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika
ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo.(Picha
na Ikulu)
WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Usimamizi wa Mali ya Asili
na Mabadiliko ya Tabia Nchi wakitunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)
wakati wa mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali
Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)
WAHITIMU
wa Shahada ya Usimamizi wa wa Teknolojia ya Habari wakishangilia wakati
wa kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
(SUZA ) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya
Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed
Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...