MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewahakikishia wananchi wa Kata ya Pera na Chalinze kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za migogoro ya Ardhi katika Halmashauri hiyo wakati wa ziara ya kukutana na kuwashukuru Wananchi wa jimbo lake kufuatia Ushindi mkubwa walioupata katika Jimbo hilo.

Akiongea na wananchi wa Kata ya Pera , Mbunge aliwahakikishia wananchi kuwa wamejipanga vizuri kumaliza kero za mipanga hasa ile isiyokwisha kati ya Kitongoji cha Pingo na Chamakweza ambao umedumu kwa takribani miongo Miwili.

Awali akiwa katika Kitongoji cha Pingo, Mbunge aliweza kufanya mkutano wa wazi na Wananchi ambapo pia aliongozana na watalaam mbalimbali wa Idara pamoja na viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Kata na Wilaya wakiwemo Wanasiasa.

Mbunge amewaahidi Wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano huku akiwashukuru kwa kukichagua kura nyingi Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwemo kumpatia asilimia zaidi ya 94 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Katika mkutano huo ambao Mbunge alipokea pia kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwemo migogoro wa mipaka,Mgorogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, Fursa za TASAF, mikopo ya Jamii , Afya na mengineyo.

Hata hivyo Mbunge aliweza kutolea ufafanuzi baadhi ya kero za Wananchi ambazo zimeanza kufanyiwa kazi na kuwakumbusha kuwa serikali haikuwa imelala ilikuwa inafanya kazi,  huku zingine akiahidi kuzichukua kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.




 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...