Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza na Wahitimu pamoja na Wageni katika Mahafali ya 44 ya Taasisi ya Ustawi Wa Jamii Jijini Dar es salaam. Mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wakuu wa Idara za Taaluma za Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika Mahafali ya 44 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
Wahitimu mbalimbali katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kwenye Mahafali ya 44.



Na Khadija Seif, Michuzi TV.
WAHITIMU katika Taasisi ya Chuo Cha Ustawi wa Jamii Waaswa Kusaidia jamii na kusuluhisha Migogoro katika Nyanja mbalimbali kupitia Mafunzo waliyopewa chuoni hapo.
Akizungumza hayo Katibu Mkuu Wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James katika Mahafali ya 44 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakati akiwatunikia vyeti waliohitimu fani mbalimbali ikiwemo Cheti Cha Msingi katika Kazi za jamii kwa Vijana na Watoto amesema Ngao ya uongozi bora wowote ule Kimisingi ni lazima uguse swala la Elimu.
"Serikali inatambua mchango Mkubwa unaopatikana katika Elimu hasa chuo hicho kwani ndio Misingi Mikuu katika uwajibikaji mzuri makazini na katika Jamii inayowazunguka kutokana na kuzalisha wanataaluma wazuri wenye Masilahi ya kulikomboa taifa.
Hata hivyo James ameeleza kuwa kwenye mafanikio yoyote hapakosi changamoto ndogo ndogo.
"Chuo hichi kina matatizo ya Miundombinu hivyo ni wakati Sasa Serikali kuyapokea matatizo hayo na kuyapatia ufumbuzi na nikiwa Kama mgeni rasmi nahaidi kuyatekeleza na nimewasihi waje katika Wizara yetu ya Fedha na Mipango tuongee kwa upana".
Pia amewataka Wahitimu hao Kusaidia jamii zao kuanzia ngazi ya Kata,Wilaya hadi kwenye Halmashauri kutokana na ujuzi ambao tayari wameupata.
"Kimsingi wajiandae kujitolea kwenye jamii zao na kusuluhisha matatizo yao."
Kwa upande wa Muhitimu katika ngazi ya shahada katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Moile Loorbuluka amesema elimu waliopata chuoni hapo iwe yenye manufaa na tija kwa mustakabali wa Taifa.
"Tumetumia muda mwingi kuchukua mafunzo chuoni na vipo vya Msingi tumejifunza na viapo vyetu ni kusaidia jamii kwa asilimia zote."
Hata hivyo ameiomba Serikali kutoa nafasi za ajira ili Elimu hiyo waliopata iwafikie walengwa hasa watu wa vijijini ambao bado changamoto za elimu haijafika kwa asilimia zote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...