Baadhi ya bidhaa ambazo zimetengenezwa na wanawake wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali zimepangwa kwenye meza.

Mkaa mabadala uliotengenezwa na baadhi ya wajasiriamali kwa kutumia takataka mbalimbali baada ya kupata elimu ya kutengeneza mkaa huo kutoka FORUMCC.

Mjasriamali Judith Mabere kutoka kikundi cha Mwashitegasi mkoani Mwanza akizungumzia umuhimu wa elimu ya ushonaji ambayo wanapatiwa na FORUMCC.

 

Baadhi ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya ujasiriamali wakiwa katika Ofisi z FORUMCC wakisubiri kuanza kujengewa uwezo kuhusu masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi hasa kuangalia namna ambavyo wanaweza kutumia fursa zilzopo katika kujiingiza kipato.

 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAJASIRIAMALI kutoka vikundi mbalimbali vya wanawake wametoa pongezi kwa Shirika la FORUMCC kwa kuwapatia elimu ya mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo hivi sasa wanaitumia elimu hiyo kutengeneza uchumi na kujiinua kimaisha.

Wametoa pongezi hizo wakiwa katika ofisi za FORUMCC zilizopo Salasala jijini Dar es Salaam ambako wamekuwa wakipatiwa elimu ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi hasa katika kuhakikisha wanatumia elimu wanayopewa kuitumia kama fursa za kujipatia fedha.Miongoni mwa elimu ambao wamepewa wajasiriamali hao ni kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zinatokana na takataka,ushonaji na ujasiriamali.

Mjasiriamali Agness Daniel kutoka kikundi cha Wajasiriamali cha Fahari Yetu amesema kutokana na elimu ambayo wamepatiwa na FORUMCC kwa sasa wanatengeneza mkaa badala, wanatenegeneza mbolea inayotokana na takataka laini kama maganda ya ndizi na mabaki ya chakula.

"Kutokana na mabadiliko ya tabianchi tumejifunza kila kilipochopo mbele yetu kwetu sisi ni fursa ,takataka yoyote kwao ni fursa, chochote ambacho kinatupwa tunaokota.Kwanza tunawashukuru FORUMCC kwa kutuwezesha vifaa vya kuwekea taka ambavyo wanavitumia kutenganisha taka ngumu, taka zinazooza na zile ambazo haziozi.

"Kama kopo za plastiki tunatenganisha tunaziuza tunapata fedha, mabaki ya vyakula tunachanganya pamoja tunatengeneza mbolea kwa kuchimba mashimo na tunufukia baada ya mwezi tunafukua inakuwa mbolea.Pia tunatengeneza mboji ambayo yenyewe hatufukii chini tunachukua kama nyasi za maji ambazo tunaziweka kama matuta na baada ya siku 20 inakuwa mboji.

"Tunatengeneza tunatengeneza mkaa mbadala kwa kutumia takataka za aina zote , tunachukua taka tunachoma na kutengeneza mkaa ambao unatumika masaa mengi, mkaa huu wakati wa kuutengeneza tunachanganya na uji wa unga wa muhogo.Mkaa  ule unaweza kuutumia kwenye vifaranga, mkaa wetu unaweza kutumia jiko moja tu ukapika na kuunga maharagwe na bado ukautumia kupikia vyakula vingine,"amesema.

Pia amesema kupitia elimu ambayo wameipata kutoka FORUMCC wanatengeneza vyungu vya maua, sabuni , jiki, batiki pamoja na majini ya chai, ambavyo hivyo vinatengenezwa kwa kutumia vitui vingine.Ametoa rai kwa akina mama kuhakikisha wanaendelea kulinda mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha Burudoza kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam Catherine Luambano kikundi chao wapo wanawake 32 na kimesajiliwa."Kkwanza napenda kuwashukuru FORUMCC ambao wametutoa mbali , kitu cha kwanza wametupa elimu ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

"Katika maeneo ambayo tulikuwa tunaathirika na mabadiliko ya tabianchi ni Vingunguti , tulikuwa hatuelewi, maji yalikuwa yanajaa mpaka ndani kutokana na miundombinu lakini tulikuwa hatuelewi na hivyo tukawa tunailaumu tu Serikali, tunafahamu  Serikali imetengeza mifereji na wananchi wanakwenda kumwaga takataka na kuziba chemba lakini bado tunapeleka lawama kwa Serikali.

"Lakini baada ya elimu ya FORUMCC akina mama tukaweza kukusanyika na kila Jumanne tunafanya usafi, tunazibua mifereji na hata kama mvua zinanyesha bila mpangilio lakini ratiba ya usafi ipo,awali maji yalikuwa yanaingia ndani lakini kutokana na elimu ambayo tumepewa sasa maji hayaingii, labda yaingie kwa bahati mbaya maana mifereji ni misafi.

"Hivyo tunawashukuru sana FORUMCC, pia wametupa uwezo wa kujiongezea kipato, wametupa elimu inayotuwezesha kutengeneza mbolea kwa kutumia takataka laini , sisi kabla ya FORUMCC takataka tulikuwa tunajaza katika kiroba kimoja lakini baada ya elimu tunatenganisha taka, zile taka ngumu tunasubiri gari inakwena kumwaga na taka laini tunachukua tunatengeneza mbolea,"amesema.

Amefafanua  wanachukua takataka hizo na kuchimbia chini na baada ya mwezi mmoja mbolea inakuwa tayari na wateja wao wakubwa ni wakulima wa mbogamboga katika bonde la Msimbazi."Mpaka sasa tunashukuru Serikali imetupa mkopo tumepata eneo jingine Viwege kwa hiyo sisi tunatengeneza mbolea na wakati huo huo ni wajasiriamali.

"Tunawateja wengi sana wa mbolea, lakini elimu yote ni ya FORUMCC ambayo imetuwezesha kuwa na njia nyingine za kupata fedha,pia tunatengeza mito ya kulalia, tunakwenda kwenye viwanda kuna taka nzuri ambazo zinabakia, tunakwenda kiwanda cha NIDA tunanunua vitambaa ambavyo tunatengeneza foronya za kulalia , uchafu unaobaki tunatengeneza makanyagio kusafishia miguu,"amesema.

Ametoa rai kwa wanawake badala ya kukaa nyumbani na wengine vibarazani wakipiga soga, ni vema wakajiunga kwenye vikundi ili kuweza kupata elimu ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi ambayo itawafanya wawe na shughuli za kufanya na kuingiza kipatapo kama ilivyo kwa wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...