SERIKALI imewahimiza walimu kutekeleza majukumu yao kwa wepesi zaidi ili kuongeza nguvu katika sekta ya elimu katika halmashauri mbalimbali kote n
chini.

Pia imesema kuna kila sababu ya walimu kuendelea kuwa raia  wema wenye kufanya kazi kwa weledi  na kuhakikisha  wanaepuka uzembe,udanganyifu,rushwa  na vitendo vya ufisadi hususani katika kipindi hiki cha awamu ya pili cha Rais John Pombe Magufuli katika utendaji wao wa kazi.

Naibu Katibu  Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Gerald Mweli, ameyasema  hayo wakati wa Mahafali ya 56 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Kampasi Kuu ya Dar es Salaam, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Joo jijini Dar es Salaam

Amesema elimu ni vitendo, uteuzi au promotion unaangalia utendaji kazi sio vyeti. Mtu anasifiwa kutokana na kile anachotoa hivyo chuo kitapata heshima yake kutokana na kile kitakachozalishwa.

Aidha, Mweli amesema  Serikali kupitia OR-TAMISEMI  na WyEST imeingia makubaliano na Benki ya Dunia kutekeleza mradi wa miaka mitano wa kuimarisha Ubora wa sekondari nchini na pia itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW) katika kuhakikisha inasimamia  kikamilifu Mkakati wa kitaifa wa kisomo na elimu kwa umma kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa Amesema utekelezaji huo pia utaweza kusaidia kupunguza tatizo la watu kutojua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK) tatizo ambalo lipo  katika jamii 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dk. Michael Ng’umbi amesema wahitimu 1,786 waliohitimu masomo yao wametoka katika kampasi tatu, ya Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza ambapo kati yao wahitimu 121 ni wa shahada, wengine 1599 ni wa stashahada na 66 ni wa Astashada .
Amesema katika mwaka huu  wa masomo 2019/2020 wahitimu 1498 kati yao, 322 wmaesoma kwa njia ya ujifunzaji wa kawaida na 1176 wanasoma kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa kutoka katika vituo 51 vya mafunzo.

Amesema wahitimu waliotunukiwa vyeti wameandaliwa kuwa walimu na viongozi wasimamizi wa  programu za elimu ya watu wazima huku pia wakiwapo walioandaliwa kusimamia programu za maendeleo ya jamii na mambo mtambuka.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi la Taasisi hiyo, Dk. Naomi Katunzi amewapongeza wahadhiri na watumishi kwa kutimiza wajibu wao  katika kutekeleza majukumu yao na kuongeza kuwa Taasisi imekuwa ikipata mafanikio mbalimbali ikiwemo kukamilisha uandaaji na kuzindua mkakati wa miaka mifano wa kisomo na elimu  kwa umma,kuongeza  fursa za upatikanaji wa elimu na mafunzo hasa katika ngazi ya stashahada. 

"Bila shaka utendaji wenu wenye tija ndio uliosababisha kupatikana kwa wahitimu hawa 1498 hapa kampasi kuu ya Dar es Salaam waliotufanya tukusanyike mahali hapa siku hii kuheherekea mahafali yao,"amesema.

Aidha amewapongeza wahitimu wote kwani pamoja na changamoto nyingi walizokabiliana nazo zikiwemo za kiuchumi, kijamii na zile za kitaalum wameweza kukabiliana nazo na kufika siku hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...