MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika Agri Thamani akitoa mafunzo kwa wenyeviti na wajumbe wa Viti Maalumu wa Serikali Mitaa Manispaa ya Bukoba
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani akitoa mafunzo kwa wenyeviti na wajumbe wa Viti Maalumu wa Serikali Mitaa Manispaa ya Bukoba


AFISA Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Bukoba akiishukuru Shirika la Agri Thamani kutoa Mafunzo ya kutengeneza sabuni ya Maji kwa Walimu wa Afya wa Shule zote Manispaa ya Bukoba na Wanawake wa Manispaa hiyo



MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani kushoto akishauriana jambo na waratibu wa miundombinu ya mafunzo hayo



MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika Agri Thamani kushoto akiwa na Mratibu wa Agri Thamani Kagera



Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo
Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo



MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani wametoa mafunzo ya lishe bora kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wajumbe wake kutoka Mitaa yote 66 ya Bukoba Manispaa mkoani Kagera.

Mafunzo haya yameandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba yakiwa na lengo kuhimiza suala la lishe bora kwenye maeneo yao.

Shirika la Agri Thamani limeamua kutoa mafunzo haya ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha kuwa Viongozi hawa wanachangia ipasavyo katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhe Neema Lugangira amesema kwamba kwa awamu ya kwanza Mafunzo hata yatatolewa kwenye Serikali za Mitaa za Wilaya zitakazochaguliwa kutoka Mikoa mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo yamewanufaisha viongozi 312 na kupitia Ushiriki wao kama Viongozi kuanzia Ngazi ya Jamii huku akieleza Agri Thamani ina amini kama Taifa tutaweza kufikia lengo la kuimarisha lishe bora nchini kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...