Kufuatia
taarifa zinazo sambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu askari wa
mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA kumuua Simba katika
kijiji cha Ngwala wilayani Songwe ili kunusuru maisha ya watu na
kuonekana kuwa wamekiuka haki za wanyama na kuleta mjadala katika
mitandao ya kijamii mamlaka hiyo imetoa ufafanuzi kwamba ilikuwa
inatekeleza majukumu yake.
Akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari afisa wanyamapori mwandamizi udhibiti wa wanyamapori
wakali na waharibifu TAWA Wilbright Munuo, amesema mamlaka inakeme
vikali taarifa za opotoshaji zinazo sambaa kwenye mitandao ya kijamii
kuhusu udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu.
Amesema
jamii inatakiwa kufahamu kuwa kazi zinazofanywa na wataalam wa TAWA
zinafanywa kwa kuzingatia sheria ya uhufadhi ya wanyamapori namba 5 ya
mwaka 2009, hivyo hazipaswi kubezwa kwani kufanya hivyo ni kuingilia
majukumu ya mamlaka.
Aidha amesema sheria ya
uhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 inatambua umuhimu wa kulinda
maisha ya watu na mali zao dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu,
licha ya mamlaka kutumia mbinu mbalimbali za kuthibiti wanyamapori hao
katika vijiji ikiwemo kutishia kwa risasi.
Pia
amesema njia nyingine zinazotumika ni kuwapeleka wanyama wakali na
waharibifu katika bustani na ranchi za wanayapori kwa kuzingatia
mahitaji Ili kuepusha taharuki kwa wananchi.
Amesema
mamlaka katika kuhimarisha usalama wa maisha ya watu na mali zao
imekuwa ikihamisha wanyamapori waliokuwa wakivamia maeneo ya wananchi na
kuwarudisha katika maeneo ya hifadhi.
‘‘Mwezi
mei,2017 Tembo wanne walivamii maeneo ya chuo kikuu cha dodoma
waliwarudisha hifadhini bila ya kuleta madhara kwa wananchi,pia mwezi
February 2020 TAWA kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa wanyamapori
Tanzania TAWILI tuliwahamisha Simba 36 ambao waliua ng`ombe zaidi ya
100 katika Vijiji cha Kwitete,makundusi,iharara, robanda,pakinyigoti,nichoka na maeneo ya hifadhi ’’Alisema Wilbright Munuo.
Vilevile
Munuo ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2020 pekee
jumla ya matukio 993 ya wanyamapori kuvamia maeneo ya wananchi
yaliripotiwa katika vituo vya TAWA ambapo wanyamapori hao walirudishwa
kwenye maeneo ya hifadhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...