Mkurugenzi na Muasisi wa Meadows Academy Mohamed Arif Suleman akizungumza kuhusiana matembezi ya Uhuru ya Kilomita 10.3 yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Oasterbay Daud Joseph akizungumza kuhusiana na matembezi hayo yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi Christina Mpili akizungumza namna walivyoshiriki matembezi ya Uhuru yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi na walimu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza matembezi ya Kilomita 10.3 yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.
Mwalimu akiwa katika Pamoja mara baada ya kufanya matembezi ya Kilomita 10.3 yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya walioshiriki Matembezi ya Uhuru yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Muasisi wa shule ya Awali ya Meadows Academy Mohamed Arif Suleman akizungumza na walimu mara baada ya matembezi ya Uhuru yaliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.

*Suleman aahidi kuendelea kuratibu matembezi ya Uhuru.

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

 WAFANYABIASHARA wameombwa kusaidia sekta ya elimu kwa wanafunzi wa awali katika kuwajengea uwezo  wa kujifunza lugha ya  kiingereza ili wanapofikia elimu ya juu kuwa na uelewa ikiwa ni Pamoja kuwaweka kiushindani katika wa usaili wakati wanaomba kazi inayohusisha lugha hiyo.

Hayo aliysema Mkurugenzi na Muasisi wa shule ya Awali ya Meadows Academy Mohamed  Arif Suleman wakati wa matembezi ya Uhuru yaliyofanyika umbali wa Kilomita 10.3 katika Barabara za Masaki  jijini Dar es Salaam.

Katika matembezi hayo wanafunzi wa Sekondari na msingi walikuwa wanajibu maswali yanayoaulizwa kwa njia ya mtandao kwa kutumai simu janja.

Suleman  amesema matembezi hayo ni ya mara ya sita tangu kuanzishwa kwa kushirikisha shule za mbili za Sekondari na Msingi ambazo Sekondari ni Oasterbay pamoja na Bongoyo.

Amesema kwa kutambua watu wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto walishirikisha vituo viwili ambavyo ni Mazila na Ophanage  Of Good Hope.

Aidha amesema katika kutambua kwa kundi hilo huchukua watoto wawili katika shule hiyo pamoja na kusaidia baadhi ya shule vitabu na mahitaji mengine kwa kuamini wanawajibu wa kushirikiana na jamii.

Naye mwanafunzi wa shule ya Sekondari  Oasterbay kidato cha Tatu Daud Joseph amesema katika matembezi hayo wamejifunza vitu vingi ikiwemo na kujenga mwili kiafya.

Amesema kuwa wanashukuru matembezi hayo yanayoratibiwa kwa kuwa na vitu  vya kujifunza masuala ya teknolojia.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Christina Mpili amesema kuwa waandaji waendelee kuwashirikisha kwani wanakutana na wanafunzi wengi kutoka shule mbalimbali.

*Suleman aahidi kuendelea kuratibu matembezi ya Uhuru.

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

 Wafanyabiashara wameombwa kusaidia sekta ya elimu wanafunzi wa awali katika kuwajengea uwezo  wa kujifunza lugha ya  kiingereza ili wanapofikia elimu ya juu kuwa na uelewa ikiwa ni Pamoja kuwaweka kiushindani katika wa usaili wakati wanaomba kazi inayohusisha lugha hiyo.

Hayo aliysema Mkurugenzi na Muasisi wa shule ya Awali ya Meadows Academy Mohamed  Arif Suleman wakati wa matembezi ya Uhuru yaliyofanyika umbali wa Kilomita 10.3 katika Barabara za Masaki  jijini Dar es Salaam.

Katika matembezi hayo wanafunzi wa Sekondari na msingi walikuwa wanajibu maswali yanayoaulizwa kwa njia ya mtandao kwa kutumai simu janja.

Suleman  amesema matembezi hayo ni ya mara ya sita tangu kuanzishwa kwa kushirikisha shule za mbili za Sekondari na Msingi ambazo Sekondari ni Oasterbay pamoja na Bongoyo.

Amesema kwa kutambua watu wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto walishirikisha vituo viwili ambavyo ni Mazila na Ophanage  Of Good Hope.

Aidha amesema katika kutambua kwa kundi hilo huchukua watoto wawili katika shule hiyo pamoja na kusaidia baadhi ya shule vitabu na mahitaji mengine kwa kuamini wanawajibu wa kushirikiana na jamii.

Nae mwanafunzi wa shule ya Sekondari  Oasterbay kidato cha Tatu Daud Joseph amesema katika matembezi hayo wamejifunza vitu vingi ikiwemo na kujenga mwili kiafya.

Amesema kuwa wanashukuru matembezi hayo yanayoratibiwa kwa kuwa na vitu  vya kujifunza masuala ya teknolojia.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Christina Mpili amesema kuwa waandaji waendelee kuwashirikisha kwani wanakutana na wanafunzi wengi kutoka shule mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...