Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akitoa maelekezo alipokagua mradi wa dampo la
taka ngumu katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua bwawa la majitaka lililopo mradi wa
dampo la taka ngumu katika eneo la lililopo Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani
Geita.
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira,) Mhe. Mwita Waitara ametoa wiki mbili kwa Ofisi ya Mkoa wa Geita kufanya
ukaguzi kuhusu mradi wa dampo la taka ngumu kutokana na kujengwa chini ya
kiwango tofauti na gharama halisi.
Waitara ametoa maagizo hayo leo Desemba 28, 2020
alipofanya ziara katika eneo la mradi huo uliopo katika Halmashauri ya Mji wa
Geita ambao umetumia takriban sh. bilioni 1.9 huku ukiwa bado haujakamilika
wala kukabidhi kwa Halmashauri hiyo.
Alisema Serikali hautawavumilia wanaokwamisha miradi na
kusababisha hasara na kuagiza mkandarasi huyo atafutwe na arudishwe katika eneo
hilo ili akamilishe mradi au arudihe fedha.
“Katibu Tawala wa Mkoa naagiza mfanye ukaguzi ndani ya
wiki mbili tumpate mchawi wa mazingira na mnipe ripoti nani alihusika, nani
alisaini mkataba, fedha zilitumikaje, alilipwa nani na kwa kazi kazi, hatuwezi
kuvumilia vitendo hivi, hii ni hujuma kwa Serikali,” alionya.
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Afisa Mazingira wa Mji
wa Geita, Albert Kashaga alisema yapo mapungufu yaliyojitokeza yakiwemo ujenzi
wa kisima kimoja cha kufanya ufuatiliaji badala ya vitatu kwa mujibu wa
mkataba.
Mapungufu mengine ni kutokuwepo kwa mitambo ya kuendeshea
dampo wala mzani wa chini kwa ajili ya kupima uzito wa magari yanayoingia
kupeleka taka na kuzimwaga.
Pia Kashaga alibainisha kutokuwepo kwa eneo la kutosha linalozungka
dampo hilo ambalo lilipaswa kuwa na urefu wa mita 250 katika pande zote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...