Wakulima wapatao 21,000 kutoka katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba wanatarajiwa kunufaika na mradi wa kukuza kilimo cha mbogamboga,matunda pamoja na viungo (Viungo Project) katika shehia zaidi ya 50 Unguja na Pemba unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) wenye gharama ya Euro milioni 5.

 Hayo yamelezwa na meneja utafiti na ufuatiliaji wa mradi huo Ally Mbarouk wakati alipokua akizungumza na maafisa wa halmashauri katika ukumbi wa halmashauri ya magharib B Unguja.

 Alisema mradi huo wa miaka minne unaotekelezwa na TAMWA-Zanzibar,Jumuia ya kuhifadhi mazingira Pemba (CFP) pamoja na taasisi inayojihusisha maendeleo ya watu kutoka Dar es Salam (PDF) unalenga kuhamaisisha zaidi kwenye kilimo kilichobora kwa maslahi ya wote.

 Alisema mradi huo utatekelezwa katika wilaya tisa za Zanzibar tano kutoka kisiwa cha Unguja na nne kutoka kisiwani Pemba ambapo maeneo yote yamezingatia mashauriano ya watalamu wa wizara ya kilimo.

 Alisema miongoni mwa malengo makuu ya mradi huo ni kuwaleta karibu wadau wote  wanaohusika na uzalishaji wa mazao mbali mbali,sambamba na kuongeza ubora wa uzalishaji kwa bidhaa za kilimo pamoja  na kuongeza lishe na uhakika wa chakula kwa wakulima visiwani hapa.

 Sambamba na hayo alisema pia mradi huo utaongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa ikiwemo kuboresha masoko ya nje na ndani ya Nchi ambapo imebainika kwa miaka mingi bidhaa za Zanzibar zimeshindwa kufanya vizuri katika masoko ya nje ya Nchi.

 Akitaja  baadhi ya mikakati ambayo wamekusudia ni pamoja na kutoa elimu ya kilimo bora kisichotumia mbolea zenye madhara kwa walaji kwa kuwa watu wengi hivi sasa wamekua wakikataa  bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia mbolea isiokidhi vigenzo.

 Katika hatua nyengine afisa huyo amesema  tayari kupitia washirika wao kwenye mradi huo taasisi ya kimataifa inayojihusisha na uhifadhi wa misitu (CFI) yenye makaazi yake Nchini Canada wamekusudia kukuza soko la bidhaa za Zanzibar katika mataifa mbali mbali ulimwenguni kote kwa lengo la kutoa fursa zaidi.

 Aidha aliwataka maafisa wa halmashauri na wale wengine wote watakaohusika kwa namna moja au nyengine katika utekekelezaji wa mradi huo kutoa mashikiriano ya kina kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 Sambamba na hayo alisema anaamini kuanza kwa mradi huo kutakwenda kufunga fursa kubwa zaidi na kuinua uchumi kwa wananchi walio wengi ukizingatia kasi ya maendeleo ya uwongo zi wa amawamu ya nane inayoongozwa na Dkt,Hussein Ali Mwinyi.

 Miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja walisema mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo Zanzibar wananchi walio wengi wanahitaji maedeleo.

 Kwa upade wake Nahla Abdulhalim Mhamed ambae ni afisa wa maswali ya mtambuka kutoka Baraza la mji kaskazini B amesema ujio wa mradi huo utakua mkombozi mkubwa kwa wakulima wa Zanzibaer na wananchi wa kawaida.

 Alisema matarajio ya walio wengi kupitia mradi huo utakwenda kuongeza kipato kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

 ‘’Matarajio ya wananchi walio wengi hususani katika kipindi hichi cha uongozi wa awamu ya nane ni maendeleo na kilimo ndio sekta muhimu kwenye Nchi yetu’’aliongezea.

 Nae Makame Kitwana Makame msaidizi mkurugenzi kilimo maliasili na mazingira wilaya ya kati Unguja alisema mradi huo iwapo utatekelezwa vyema utaleta manufa amakubwa kwa wananchi walio wengi.

 Alisema kwa miaka mingi wakulima wa Zanziabar wamekua wakizalisha mazao lakinji si kwa kiwango bora na kupelekea bidhaa hizo kukosa thamani ndani na hata nje ya Nchi.


Meneja wa ufuatiliaji na tathmini kupitia mradi wa Viunga Ally Mbarouk akifafanua jambo kwa maafisa wa halmashauri tofauti Unguja wakati walipokua wakipatiwa eleimu dhidi ya mradi huo ambao.

Miongoni mwa washiriki wa mradi wa viungo kutoka katika ofsi mabli mbali za halmashauri Unguja wakifuatilia uwasilishwa wa taarifa za awali kuhusu mradi wa viungo.

Makame Kitwana Makame msaidizi mkurugenzi kilimo maliasili na mazingira wilaya ya kati Unguja  akiuliza suala kuhusu utekelezaji wa mradi wa viungo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...