======= =========
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHUO Kikuu Ardhi (ARU) kimewatunuku tuzo mbalimbali wanafunzi 87 waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika Desemba 11,2020 chuoni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga ameseama tuzo hizo zinalenga kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine ili waendelee kuweka juhudi kwenye masomo yao waweze kupata ufaulu wa juu.
Amesema sherehe hizo zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali kwa miaka kadhaa kwa kujitolea ufadhili wa hali na mali kwa wanafunzi waliofuzu kupata tuzo hizo.
Pia amewashukuru wafadhili hao na kuwaomba waendelee kuunga mkono jitihada za wanafunzi hao kwani zawadi hizo zimekuwa zikisaidia kuongeza mitaji ya utendaji kazikwa wanafunzi wa chuo hicho wanapomaliza chuo.
Ameongeza kuwa miongoni mwa zawadi zinazotolewa na wafadhili hao zimekuwa zikiongeza tija kwenye maisha ya wanafunzi kielimu na kiuchumi na kwamba kati ya hao 87 44 ni Wavulana na 43 ni wasichana.
"Mwanafunzi aliyeibuka mshindi wa julmla mwaka huu ni msichana ambapo wasichana wanaongoza kwa mwaka mwingine tena mfululizo ikizingatiwa kuwa wasichana ni asilimia 39 tu ya wanafunzi waliopo chuoni hapo.
“Kwa niaba ya uongozi wa chuo napenda kuwapongeza wote waliopewa tuzo na nawasihi waendelee kuweka juhudi kwenye masomo yao ili waje kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wenzao na jamii kwa ujumla hongereni sana na nawatakia kila la kheri kwenye masomo yenu,” amesema Profesa Kasenga.
Profesa Kassenga amesema, kesho Jumamosi kutakuwa na wahitimu 930 wa chuo hicho wa shahada mbalimbali na aliwapongeza wanafunzi kwa kufanya vizuri kitaaluma.
Alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma na kwamba hiyo ni ishara kwamba kwenye juhudi mafanikio hupatiana na akisema kuwa ni matumaini ya chuo kuwa wataendeleza jitihada hizo kwenye ujenzi wa taifa.
Baadhi ya washindi ni Mbonaga Siraji aliyeshinda zawadi zawadi saba, Mfuru Benson zawadi 2, Hyera Maria tuzo mbili, Ngenge Clara tuzo tatu.
Kwa upande wake, mhitimu bora upande wa wasichana, Cythia Charles amesema kujituma na kujali ratiba za masomo ndiyo siri kubwa ya mafanikio yake.
“Kusoma kwa bidii kuachana kabisa na starehe nidhamu na usikivu ndiyo siri pekee ya mafanikio ya kitaaluma nawaasa wanafunzi wenzangu kwamba wakizingatia haya watafika mbali kitaaluma,” alisema Cynthia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...