Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe.Festo Sanga

WANANCHI wa Kijiji cha Ndapo katika Kata ya Kinyika wilayani Makete mkoa wa Njombe wameiomba serikali na Mbunge wao kuharakisha kufikisha umeme katika taasisi za Umma kama shule, hospitali na makanisa ili kufanya watoa huduma wakiwemo walimu kushawishika kufika katika kijiji hicho kufanya kazi.

Wamesema kuna baadhi ya watumishi wakiwemo  baadhi ya walimu wakipangiwa katika kijiji hicho wanakataa kwenda kufundisha kwasababu hakuna umeme.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Iwale Asifiwe Mahenge amesema wanaomba sana umeme ufike katika sehemu hizo za taasisi kinyume na hapo wataendelea kuwanakosa walimu kufika hapo.

"Walimu wanauliza kuna umeme shule hiyo ili niende,tukisema umeme haupo basi anaamua kwenda kwenye shule zingine ambazo umeme upo tunaomba Mbunge na diwani watusaidie kupatikana umeme ufike shule ya msingi iwale na sekondari ya Kinyika" 

Kwa upande wake Mbunge wa Makete Festo Sanga amesema mkandarasi aliyepewa zabuni ya kusambaza umeme wilayani humo bado hajafanya vizuri kwani kuna vitongoji vingi havina umeme na kata zaidi ya Nne havijafikiwa na umeme.

Hivyo ambaye ni mbunge wao atafikisha kero hiyo kwa Waziri wa Nishati kuona atakavyosaidia ili mkandarasi aende haraka kusambaza umeme kwani makao makuu ya kijiji kua na umeme bila vitongoji si sawa kwani amna kijiji bila kitongoji.

Awali Msimamizi wa mradi wa REA kwa wilaya ya Makete David Jekela amefafanua sababu ya nguzo za umeme kutofika katika taasisi za umma ambapo mpimaji hakufanya kazi yake vizuri kwani kuna sehemu eneo la kazi kaweka nguzo zifike lakini katika ramani ambayo yeye amekabidhiwa na mkandarasi wa mkoa hazipo hivyo kufanya nguzo alizopewa zisifike sehemu muhimu na hivyo anamalizia kupima tena ili afikishe ni nguzo ngapi zinatakiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...