ZAKHIA Suleiman Mwalukuta ni binti mjasiriamali aliyejikita katika uuzaji wa bidhaa za urembo na vipodozi (vinavyotengenezwa kwa rasilimali asilia,) ambayo kwa kiasi kikubwa biashara hiyo imemwongezea kipato ambacho kinasukuma maisha yake ya kila siku.
Akizungumza na Michuzi Blog Zakhia amesema kuwa, amekuwa akishiriki makongamano mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa yamempa mwanga na kukuza zaidi biashara yake ya kutengeneza sabuni mbalimbali zikiwemo za mchele na kahawa pamoja na mafuta ya nywele.
Amesema kuwa ni vyema vijana wakatumia fursa mbalimbali zinazijitokeza na kuweza kujitengenezea kipato binafsi.
"Fursa zipo, tuzitumie...mimi huwa nashiriki mafunzo mbalimbali yanayoongeza ujuzi na tunawafundisha wengine ili tuweze kuyafikia Maendeleo." Amesema.
Vilevile amesema, kwa sasa ushirikiano kutoka kwa Serikali ni mkubwa hasa katika suala zima la viwanda na kupitia hilo wajasiriamali wengi watanufaika kupitia mnyororo bora wa ujenzi wa Taifa la viwanda.
Hadi sasa Zakhia ameshiriki na kupata tuzo mbalimbali katika makongamano yakiwemo ya 'Motherhood Women Connecting Gala' na 'African Women Success.'
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...