MKUU wa Wilaya ya Arusha  Kenani Kihongosi amkamata Askari Polisi aliyekuwa akiiba umeme wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO,)mbao alijiunganishia kinyume na sheria na kuweka swichi chooni ambayo ndio ilikuwa inatumika kuiba umeme huo na kupelekea kukwepa kulipa bili ya Umeme.

 Pia baada ya kumpekua katika Nyumba  anayoishi pamoja na gari yake binafsi wamemkamata na Box za Viroba vya Konyagi ambavyo vilipigwa marufuku na Serikali, lakini yeye amekuwa akivitumia kwa Kujaza katika chupa za konyagi na kuziuza kwa wananchi katika baa yake, pia wamekamata Kete za Bangi 20 ambazo alizihifadhi vizuri katika pochi maalumu na kuzificha katika gari yake, 

Pamoja na hayo bado akakamatwa Gongo lita tano ambayo aliyoificha katika buti la gari yake ndogo, pia askari huyo amekamatwa na vyuma vinavyotumika katika ujenzi wa Miradi mbalimbali vikiwa vimehifadhiwa katika banda la bata kiasi cha ndoo mbili, baada ya upekuzi pia walikakamta madumu ya mafuta ya diesel yaliyojaa mafuta yaliyofichwa sebuleni kwake.

Mkuu wa Wilaya amemwagiza OCD wa Jiji La Arusha kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya Sheria ili iwe funzo kwa wengine.

Katika operation hio Mkuu wa Wilaya aliambatana na OCD wa jiji la Arusha, OCCID pamoja na meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha ambaye alifika na mainjinia wa Tanesco na Kukata umeme uliokuwa umeunganishwa darini na swichi kuwekwa Chooni kinyume na utaratibu.

Vielelezo vyote vimechukuliwa na kupelekwa kituo cha Polisi.

Aidha amesisitiza wananchi kuwa wazalendo katika Nchi yao kwani wao kama Serikali hawatamvumilia mtu yeyote na watashughulika na yeyote bila kujali cheo wala nafasi ya mtu. 

Amesema, lazima kila mwananchi aunge mkono Jitihada za Serikali kwani kila mmoja anaona namna  Rais Dkt. John Joseph Magufuli anavyopambana kuijenga nchi hii kiuchumi hivyo lazima aungwe mkono kwa kulinda miundombinu ya Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...