Na
Happiness Shayo – Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi amewataka
watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi
ili kuimarisha afya zao na kujenga mshikamano na upendo katika maeneo yao ya
kazi.
Dkt.
Kijazi ametoa wito huo wakati wa bonanza la watumishi lililoandaliwa na Wizara
ya Maliasili na Utalii lililofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma.
''Mazoezi iwe ni sehemu ya maisha yetu na pia iwe
ni sehemu ya kazi zetu² amesisitiza Dkt. Kijazi.
Ameongeza
kuwa, Wizara yake itajipanga kuhakikisha kila mtumishi anashiriki katika
kufanya mazoezi na pia kila mtumishi anashiriki kwenye mabonanza na amewataka
watumishi kuendelea kuhamasishana ili ushiriki uzidi kuongezeka katika
matamasha yanayokuja.
Dkt.
Kijazi amefafanua kuwa Wizara itaweka utaratibu wa kuwatambua washiriki bora wa
kila mwaka wanaofanya mazoezi na wanaoshiriki kikamilifu katika matamasha kama
hayo na kuwapa zawadi maalumu.
Pia,
amesema kuwa, Wizara itahakikisha ushiriki wa watumishi katika matamasha hayo
hauishii Dodoma bali utaendelea kwenye matamasha mengine yanayofanyika nchini, kama
Kilimanjaro
Marathon, Ngorongoro Marathon na Serengeti Marathon.
'' Watumishi watakaofanya vizuri tutawadhamini ili
waiwakilishe Wizara kwenye Marathon hizo.''Amesema.
Naibu
Katibu Mkuu, Dkt. Kijazi amewapongeza washiriki wote walioweza kukimbia mbio za
kilomita tano kwa kupata medali na kuwataka ambao wameshindwa wajitahidi
kipindi kijacho wamalize mbio hizo.
''Ni imani yangu kuwa bonanza linalokuja wote
tutamaliza mbio za kilomita tano, cha msingi tuendelee kufanya mazoezi ,tusisubiri
hadi matamasha haya yafike ndo tufanye mazoezi.'' Dkt. Kijazi amesema.
Dkt.
Kijazi amewashukuru Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club kwa
kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufanikisha bonanza hilo na kusema kuwa uwepo wao ni chachu kwa Wizara
katika kuimarisha mabonanza.
Naye,
Mwenyekiti wa Jogging Clubs Dodoma, Bw.Mugisha Mujungu ameahidi kuendelea
kushirikiana na Wizara kila itakapohitaji ushirikiano katika kufanya mazoezi na
kuwataka watumishi wa serikali kujiunga na Jogging Clubs ili kuimarisha afya
zao.
Bonanza
hilo limehudhuriwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na washiriki
kutoka Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club za Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...