Madiwani wa halmashauri ya Arusha wakifatilia Kikao cha baraza .
Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Saad  Mtambule
akiongea katika Kikao cha baraza la madiwani  kilichofanyika Katika
ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo .


Na Woinde Shizza, Michuzi Tv-Arusha


HALMASHAURI ya Arusha imeeleza sababu za halmashauri hiyo  kutokufikia
lengo la ukusanyaji wa mapato kota ya kwanza  kwa mwaka 2020 kama
ilivyojiwekea  makisio ya zaidi ya billioni 59 na millioni 188 na
kufanikiwa kupata billioni 21 na millioni 837 kufika Desemba 31,2020.

Sababu hizo zimetolewa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Saad Mtambule
 wakati akisoma taarifa za mapato na matumizi kwa mwaka huo kwa baraza
la madiwani alisema kilichofanya wasifikie asilimia 100 kota ya kwanza
ni pamoja na kukosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa wafanyabishara
na kuyumba kwa bishara ya utalii.

Mtambule alifafanua kuwa walipa kodi mbalimbali wengi wanahitaji
kusukumana nao kwani ulipa kodi wa hiari umekuwa ni shida lakini kama
halmashauri wamejipanga wenyewe kama watendaji kutoka na kutembea kwa
pamoja kuhakikisha kila anayepaswa kulipa analipa na kile anacholipa
kiwe kile kinachostahili kupokea.

“Anayefanya biashara awe na leseni na alipe anachostahili na
tumekutana na hizi changamoto, wakati mwingine tunapelekana polisi
wengine mahakamani lakini ndo hivyo mapato hayana lele mama lazima
twende,” Alisema Mkurugenzi huyo.

Alieleza kuwa sehemu nyingine wamekua wakiondoa vitabu vya ukusanyaji
mapato na kupeleka mashine kama ilivyoelekezwa na serikali kwamba kila
chanzo cha mapato inakusanywa kwa kupitia mashine hizo.


Alisema changamoto nyingine ni kushuka kwa biashara ya utalii ambapo
alieleza kuwa uchumi wa Arusha unategemea  sana utalii na utalii ukifa
kwenye mahoteli biashara inaenda chini ambapo kwanzia mwezi wa pili
2020 na hii changamoto bado inaendelea idadi ya watalii iko chini.

“Watalii wanapokuja sisi ndio biashara nyingi zinachangamka  ushuru wa
huduma tupata hapo na ushuru huo ni sehemu ya mapato kwahiyo
tumekutana na changamoto hizi  lakini kuna jitihada mbalimbali
tunaendelea nazo kama watendaji na tunaamini kufikia mwezi wa nne,
watano tutakuwa tumefikia lengo tulilojiwekea,”Alisema.

Alifafanua kuwa wamebuni vyanzo vingine ambavyo vitawasaidia kukusnya
mapato mengine ambapo ni pamoja na ujenzi wa shuele ya mchepuo wa
kingereza ambayo imeshaanza kupokea wanafunzi lakini pia wanafanya
kazi ya urasimishaji kwenye kata ya Mlangarini kijiji cha Kiserian na
hadi tarehe january 25,2021 kuna watu wenye viwanja zaidi ya 3000
vilivyotambuliwa.

“Viwanja hivi ukizidisha mara laki moja na elfu hamsini utaona unaweza
ukaona ni zaidi ya millioni 400 ambazo tukizipata tukizikusanya
zitatusaidia kuongeza kiasi ambacho hakipo lakini pia kuna maeneo ya
Engorora,Laroi tutaenda na penyewe kufanya urasimishaji,"Alieleza.

Alifafanua kuwa wanaendelea kubuni vyanzo ambavyo viko kwenue maeneo
yao ambapo ni pamoja na kuja na wazo la kuanzisha kituo cha Radio
ambacho kitawasaidia kujitangaza na kuondoa changamoto ya wakazi wa
halmashauri hiyo wa mita 200 kutoka jiji la Arusha kutokuifahamu
halmashauri hiyo na kwenda kulipa mapato jiji.

“Wafanya biashara wengi waliopo eneo la mita 200 upande wa halmashauri
yetu unashangaa hawaijui halmashauri yao wanaenda kukata leseni jiji
na ukiwauliza wanakuwa hawaijui Arusha DC na ili tuweze kujitangaza
tumeona tuanzishe radio yetu na tayari tumeshaanza kulifanyia
kazi.”Alisema.

Hata hivyo alisema kwa kipindi hicho mapato ya ndani wamefanikiwa
kukusanya zaidi ya billion 2 ambayo ni sawa na asilimia 56.32 na
zingine ni ruzuku kutoka serikali kuu ikiwemo ruzuku za mishahara,
matumizi mengine, EP4R na mengineyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...