Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimkabidhi zawadi ya kinywaji cha Johnnie Walker Mkuu wa Majeshi ya Ulinzia na Usalama mstaafu Generali George Waitara ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika mchezo wa Gofu. Hafla hiyo ilifanbyika jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuhitimisha mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy 2020.
Veterani wa mchezo wa Gofu Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 1,500,000/-mshindi wa kwanza ambaye ni mchezaji wa kulipwa (profesional player) kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo Bryson Nyenza baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy yaliyodhamini na Kampuni ya Bia ya Serengeti Kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.
Baadhi ya washiriki mashindano wa Johnnie Walker Waitara Trophy 2020, wakijiandaa kwa ajili ya mashindano hayo makubwa yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu vya kijeshi vilivyopo Lugalo jijini Dar es Salaam na kushirikisha zaidi ya wachezaji 180 kutoka nje na ndani ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...