Shirikisho la Mchezo wa karate nchiniTanzania(JKA/WF-TZ)) linatarajiwa kufunguwa tawi jipya la mchezo huo katika makao makuu ya nchi jijini Dodoma siku ya kesho Jumatatu tarehe 25-01-2021.

Sensei Mikidadi Hemed Kilindo(Ganchan)ambaye ni mkufunzi wa chezo wa karate mwenye dani 4,ambaye pia ni bingwa mchezowa karate kwa Afrika Mashariki kwa miaka tano mfululizo,ndiye atakuwa Mwalimuwa klabu hiyo,iliyopo barabara ya (Iringa road) mkoani humo.

Sensei Mikidadi HemedKilindo(Ganchan)amewaomba wakazi weye umri wowote wa mkoani Dodoma kujiunga naklabu hiyo,ambapo lengo ni kueneza mchezo wa karate nchini kote Tanzania.

Shirikisho la Mchezo wa karate nchiniTanzania (JKA/WF-TZ) limekuwa na utaratibu wa kusimamia matawi kutoka mikoambalimbali nchini Tanzania,lengo likiwa ni kufundisha mchezo wa karate kwawatoto,Vijana na kwa wenye umri tofauti,kwa dhumumi la KuimarishaAfya,Kujilinda na hata kupata ajira Kupitia mchezo wa Karate.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...