SISI wasanii na waandishi wa habari tunashukuru mungu kwa kutuepusha na janga la Corona katika Nchi yetu. Katika kuendeleza hali nzuri tuliyonayo tunawaomba watanzania wote kuungana nasi katika awamu ya tatu ya KUJIFUKIZA( NYUNGU SEASON 3)

Katika awamu hii ya tatu tunawaomba Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani, Wafanyabiashara, Wanachuo, na wananchi wote kwa ujumla kuungana nasi katika NYUNGU SEASON 3.

Wiki ya KUJIFUKIZA( NYUNGU SEASON 3)itaanza  siku ya Jumamosi ya tarehe 30 January hadi tarehe 5 February 2021. Wiki hii ni muhimu sana kwa sisi watanzania kwani tunafahamu kwamba Nchi yetu ipo salama kutokana na janga la Corona hivyo tunachukua hatua hii kama njia sahihi ya kuendelea kujikinga na janga la Corona kwani Sisi tupo salama hivyo hata kama kirusi cha Corona kikitaka kujipendekeza kuingia nchini kwetu kutoka pembe yeyote ya Dunia kiweze kutokomea na kuendelea kulinda Uchumi wa Nchi yetu unaopaa kwa kasi.

Zoezi hili ni muhimu tukalifanye Watanzania wote kwa pamoja ndani ya wiki moja bila ya hata mtu mmoja kukosa ili kuonyesha umoja wetu, nguvu yetu, na dhamira yetu juu ya kuendelea kuiweka Nchi yetu kuwa salama na janga la Corona.

Sisi wasanii na waandishi wa habari tunawaomba viongozi wa Dini zote waendele na maombi ya kuliombea Taifa letu ili tuendelee kuwa salama ikilinganishwa na mataifa mengine Duniani yanayo teseka kwa  janga la Corona.

Wenzetu wanao husika na Sekta ya Utalii tunaomba muwakaribishe watalii wengi ndani ya wiki hii waje Tanzania kushiriki nasi katika NYUNGU SEASON 3 kama sehemu ya Utalii.

Wenzetu wanao miliki saloon tunawaomba muungane nasi kwa kuweka mitambo ya kujifukiza katika saloon zenu ili wateja wanaokuja kupata huduma saloon waweze kupata  starehe ya kupiga NYUNGU.

Wiki hii iendane sambamba na ulaji wa matunda yetu ya asili yakiwemo: limau, Tangawizi, Ubuyu, Ukwaju, n.k

❇️❇️❇️TANZANIA TUPO SALAMA, HATUNA CORONA, HIVYO TUENDELEE KUILINDA TANZANIA YETU, NA TUULINDE UCHUMI WETU KWA KU
ZUIA CORONA❇️❇️❇️

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nyungu Season 3 siyo kama ya season 1 and season 2. Kuna haja ya kuongeza kampeni kwa wananchi. Tuwakumbushe Covid 19 imetengenezwa maabara ni artificially made virus. Hivyo Nyungu ya mitishamba ina uwezo mkubwa sana kukisamabaratisha.Watanzania tupige Nyungu daily

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...