Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akizindua mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria itakayo hudumia miji ya Tabora, Igunga na Nzega.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akitoka kukagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji
Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony
Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji
katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora,
Igunga na Nzega
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima
wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma
ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30
Januari 2021. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Huduma ya Wagonjwa wa Dharura katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021. PICHA
NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...