MBUNGE wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara  Edward Kisau Ole Lekaita amefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika Kata ya Dongo. 

Ole Lekaita ambaye aliwasili katika Kijiji cha Dongo mnamo saa nne (4) asubuhi aliweza kupanda mlima Dongo na kwenda kukagua chanzo cha maji ambako alitembea karibu kilometa 5 kwa miguu akiongozana na Mkiti wa CCM Wilaya, Mhe. Diwani Viti Maalum kata ya Dongo, Mkiti wa CCM Kata, Katibu wa CCM Kata, Mkiti wa Kijiji cha Dongo, Mkiti wa Kijiji cha Changombe, Mtendaji wa Kata Dongo, Watendaji wa Vijiji vya Dongo na Changombe, Mkiti wa Kitongoji na Kamati ya Maji kijiji cha Dongo.

Katika ziara hiyo Mhe. Ole Lekaita alitembelea chanzo cha maji  mlimani pamoja na kutembelea sehemu inayotarajiwa kujengwa Bwawa Kubwa litakalo hudumia Kata za Laiseri na Dongo.
 Ole Lekaita vile vile alitembelea pia shule ya Msingi Dongo, Shule ya Sekondari Dongo, Shule ya Msingi Changombe na Zahanati ya Dongo.

Katika ziara hiyo  Mbunge Ole Lekaita alifanikiwa kujionea miradi mbalimbali iliyojengwa kwa nguvu za jamii pamoja na serikali. Mhe. Ole Lekaita alipokuwa mlimani katika chanzo cha maji alimpigia Meneja wa RUWASA simu na kumwomba atembelea chanzo hicho cha maji na baada ya wiki moja Mbunge ana Meneja wa RUWASA wakutane na kuzungumzia mradi huo namna ya kuboresha zaidi ili wananchi waweze kunufaika zaidi na kuweza kutatua kero ya maji ambayo imekuwa sugu katika Kata hiyo ya Dongo.

Katika ziara hiyo viongozi wa kata ya Dongo walimsifia sana Mbunge Ole Lekaita kwa kutembea muda mrefu kwa miguu na kukagua miradi hiyo kabla ya kwenda Bungeni kama alivyoahidi katika wakati wa kampeni.

" kwa kweli Mbunge tumempata, yaani tulimwambia afike Kijijini saa NNE( 4) kamili asubuhi na amefika saa nne ( 4) kasorobo kizungu kabisa. kwa hili kwa kweli Big up sana Mhe. Mbunge. Lakini vile vile kutembea kwa miguu na kupanda juu mlimani kwenda kuona chanzo cha maji ni jambo ambalo hakuna mbunge ambaye ameshawahi kufanya hiyo kwa kweli tumempata Mbunge wa kweli" alisema Mhe. Rahel- Diwani wa Viti Maluum Kata ya Dongo.

Katika ziara hiyo  Lekaita aliweza kukutana na wananchi mbalimbali njiani na kuzungumza nao.

  Lekaita alikaa Dongo kuanzia saa nne (4) asubuhi mpaka muda wa saa kumi na mbili (12) jioni kabla ya kurudi Kibaya.

"Kwa kweli Ole Lekaita ni mbunge wa aina yake. kuweza kufika na kukaa na wananchi wake muda wote ni ishara kubwa kwamba tumempata Mbunge wa kweli. Kwa kweli chama cha Mapinduzi hakija kosea kumteua Mhe. Ole Lekaita." Mkiti wa CCM Kata ya Dongo.

Mbunge huyo kwa sasa yupo Kiteto akifanya ziara mbalimbali jimboni kabla ya kwenda Bungeni kwa nia ya kujionea shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni hapo.

"Kwa kweli ni furaha yangu kutembea na kuona miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi ili kuweza kuona na kufahamu kwa undani na kujenga uelewa mzuri na mpana zaidi kuhusu miradi katika jimbo zima. Kwa kweli mimi sipendi vya kuambiwa tu bali nataka kufika kujionea mwenyewe kwa macho," amesema mbunge huyo.

Ole Lekaita ameshafanikiwa kutembelea Kata za Chapakazi na Dongo na anaendelea na ziara zake jimboni mpaka hapo Bunge litakapo anza vikao vyake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...