Mbunge  wa Mbunge wa jimbo la Kihaba Vijijini(Chama Cha Mapinduzi (CCM), Michael Mwakamo amefanya ziara na kupata taarifa ya hali ya huduma na utekelezaji wa   mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na kuona uzalishaji wa maji katika mtambo huo.

Mbunge wa Kihaba Vijijini, Michael Mwakamo, alisema kuwa jitihada kubwa zinafanya na serikali katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama hivyo wananchi wanapaswa kuwa walinzi wa miradi hiyo mikubwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja ndio aliyesema hayo leo, wakati wa ziara ya Mbunge wa Kibaha Vijijini Michael Mwakamo ya kutembelea mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na kuona uzalishaji wa maji katika mtambo huo.
“Nawahakikishia wakazi wa Dar es salaam kuwa maji ya Dawasa ni safi na salama na kwamba kwa sasa tunafanya kazi chini ya Viwango vya Kimataifa (ISO Certified) tunasubiri kuzindua cheti hicho ndani ya wiki mbili zijazo,” alisema Mhandisi Luhemeja
 “Dawa zipo na mitambo ya kisasa ipo, kwa sasa tunakamilisha ‘System’ ya uzibaji wa mabomba yaliyopasuka yanayomwanga maji kabla ya kufika kwa mteja, tukimaliza zoezi hilo nadhani mwishoni mwa mwezi ujao tutawatangazia wananchi kuwa kwa sasa maji ya Dawasa inatoa huduma ya maji safi na salama,” alisema
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kujibu maswali aliyoulizwa na Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo wakati wa Ziara yake ya kukagua miundombinu ya maji iliyopo katika Jimbo hilo.
Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo(kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja(kushoto) pamoja na maofisa wa DAWASA alipofanya ziara katika mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu katika Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoani Pwani. Ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Diwani kata ya Malandizi Euphrasia Kadala  akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kutoa changamoto za wananchi wa kata hiyo kuhusiana na masuala ya maji wakati wa Ziara ya Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo pamoja na madiwani wa Jimbo hilo kwenye mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu.
Diwani kata ya Kawawa, Alfred Malega  akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kutoa changamoto za wananchi wa kata hiyo kuhusiana na masuala ya maji wakati wa Ziara ya Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo pamoja na madiwani wa Jimbo hilo kwenye mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi sehemu moja wapo inayotumika kuchujia maji kwa Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo  pamoja na madiwani walifika kwenye Ziara ya kutembelea mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo  pamoja na baadhi madiwani waolifika kwenye ziara ya kutembelea mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi  kuhusu miradi wa mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu wakati wa Ziara ya Mbunge wa Kihaba Vijijini Michael Mwakamo pamoja na madiwani wa Jimbo hilo.
Baadhi ya mitambo iliyopo katika mtambo wa Kuzalisha maji Ruvu Juu



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...