Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
MPANGO wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) unatoa
mafunzo ya utawala bora kwa vijiji viwili vinavyoshiriki katika
usimamizi shirikishi wa misitu katika wilaya ya Namtumbo mkoa wa
Ruvuma katika kijiji cha Kilangalanga na Limamu.
Mafunzo hayo ya siku nne kuanzia tarehe 18 mwezi huu na yataishia
tarehe 22 mwezi huu, yakiwa na lengo la kuiwezesha kamati ya maliasili
ya kijiji kufahamu majukumu yao ya kila siku,wafahamu majukumu ya
serikali, wafahamu majukumu ya wadau pamoja na kujua kusimamia
,kutunza hesabu za serikali kitaalamu.
Stanley Baluweshi mwezeshaji wa mafunzo kutoka ngazi ya
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alisema katika vijiji hivyo viwili
wajumbe 10 kutoka kila kijiji wanaohusika na kamati ya usimamizi
wa maliaasili katika kijiji ndio walengwa wa mafunzo hayo.
Agnes Nchimbi mtendaji wa kijiji cha Limamu ambaye ni mshiriki wa
mafunzo hayo amedai kijiji chake kipo katika mpango wa jamii wa
usimamizi wa misitu hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kuzifahamu na
kuzifuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kuepuka migogoro
isiyo ya lazima katika jamii.
Nchimbi aliwataja wajumbe waliohudhuria katika mafunzo hayo kutoka
katika kijiji chake kuwa ni Yeye ambaye ni mtendaji wa kijiji,
mwenyekiti kamati ya maliasili,katibu wa kamati,mweka hazina ,kamanda
kamati ya maliasili pamoja na wajumbe wa 5 kutoka katika kamati
hiyo ya maliasili ya kijiji .
Kijiji cha Limamu na kilangalanga kupitia mikutano yao ya hadhara
kwa wananchi wamepitisha mpango wa jamii wa usimamizi wa misitu katika
vijiji vyao ambapo serikali kupitia mpango huo unawawezesha
wajumbe wa kamati kuwapatia mafunzo ili waweze kuusimamia vyema
mpango huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...