![]() |
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma
Chritina Mndeme amewapongeza wakulima Mkoani Ruvuma kwa kuongoza mara mbili
mfululizo kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.
Mndeme ametoa pongezi
hizo wakati anafungua Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea mjini Songea.
Akizungumzia muhtasari
wa hali ya chakula na mavuno mkoani Ruvuma kwa mwaka 2019/2021.Mndeme amesema
katika kioindi hicho mavuno yalikuwa ni tani 1,355,509 hali iliyoufanya Mkoa wa Ruvuma kuchukua
nafasi ya kwanza kitaifa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa
amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2021 mahitaji ya chakula katika Mkoa ni tani
469,172 hivyo Mkoa una ziada ya tani 886.337 na kwamba Mkoa umeendelea kufanya
vizuri katika uzalishaji wa mazao ya
Kilimo kwa mara ya pili mfululizo.
“Mafanikio haya ni
matokeo ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuendelea kujituma katika shughuli za
kilimo bila kulazimishwa na usimamizi mzuri wa maafisa ugani Ugani na viongozi
wa Serikali”,alisema Mndeme.
Mdeme ameyataja mazao
ya Ufuta,Mbaazi,na Soya kwa mwaka huu katika Mkoa Ruvuma yamefanyika kupitia
mfumo wa stakabadhi ya Mazao
ghalani hali ilisaidia kuingiza mapato
ya zaidi ya shilingi bilioni 28.
Kati ya mapato hayo,
Ufuta limeingiza zaidi ya shilingi bilioni 25,Soya zaidi ya shilingi bilioni
moja na Mbaazi zaidi ya shilingi bilioni bili.
Mndeme amesema Mkoa
unaendelea kushirikiana na Taasisi zingine za Serikali katika kusimamia zoezi
la ununuzi wa Korosho kutoka kwa wakulima ambapo hadi sasa zimeuzwa kilo
14,826,644 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 33.
Kwa mujibu wa Mndeme
msimu wa Kilimo wa Mwaka 2020/2021 Mkoa umelenga kulima hekta 672,137 za mazao
ya chakula na bustani na kuvuna tani 1,790,582 za mazao hayo.
Hata hivyo,amesema
katika msimu wa mwaka 2020/2021 serikali
itaendelea na mfumo wa bei elekezi wa kununua pembejeo za kilimo hususani
Mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA),na Wizara ya Kilimo pamoja na
Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA)imetoa bei elekezi kwa
kila Wilaya.
Mkoa wa Ruvuma ni gwiji
katika uzalishaji wa chakula nchini baada ya kuongoza katika uzalishaji kitaifa
kwa miaka miwili mfululizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...