Mndeme pia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Ruvuma kwa kufanya kazi nzuri ya kukusanya Mapato ya ndani ya Mkoa katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 sawa na asilimia 94.
“Naipongeza Halmashauri ya Tunduru kwa kukusanya Mapato ya Ndani kwa asilimia 121.87, pia naipongeza Halamashauri ya Manispaa ya Songea tangu imeanza kutumia stendi kuu ya Shule ya Tanga Januari1, 2021 imeongeza mapato kutoka shilingi 200,000 mpaka 970,000 kwa siku.” Alisema.
Mndeme amesema Mkoa unatarajia kuimarika kiuchumi kwa kuongezeka kwa mapato yatokanayo na kodi pamoja na ushuru kwasababu Barabara ya Ushoroba wa Mtwara imefunguka na kupelekea kutoa fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi.
Hata hivyo amesema biashara ambazo zinapatikana maeneo mengine Nchi Jirani za Malawi na Msumbiji yanaunganishwa kwa kupitia usafiri wa Ndege kupitia Uwanja wa ndege wa Songea na barabara ya lami ya Mtwara corridor.
Amesema Meli katika Ziwa Nyasa zimeanza kazi za Usafirishaji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Meli ya abiria ya MV Mbeya II Januari 5,2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambayo inabeba abiria 300 na Mizigo tani 200.
Hata hivyo Mndeme amewaagiza Wakurugenzi kusimamia Mapato yatokanayo na Kodi pamoja na Ushuru amesema fedha hizo hutumika katika kujenga miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya,Barabara,Ununuzi wa Ndege,Ujenzi wa Reli na huduma nyingine za kijamii.
Ameziagiza Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kubuni na kupanua wigo wa mapato kwa kuhimiza watu kudai Risiti na wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapouza bidhaa mbalimbali. Imeandaliwa na Albano Midelo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...