
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akizungumza na Mkulima Fadina Hassan pamoja na Mwenyekiti Ngonda Amcos Rashid Lingoni ofisini kwa Afisa Tarafa (hawapo pichani) wakati akitoa maelekezo ya kukamatwa kwao.
Na Mwandishi wetu Mihambwe
AFISA Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu ameagiza kukamatwa kwa uongozi wa bodi nzima ya chama cha msingi cha Ngonda kufuatia upotevu wa gunia 10 za Wakulima.
Shilatu ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu Januari 18, 2021 kufuatia lalamiko lililoletwa kwake na Fadina Hassan aliyelalamika juu ya kutokulipwa kilogram 100 alizopima ghalani tangu Oktoba 23, 2020 ambapo Mwenyekiti wa Ngonda Amcos Rashid Lingoni alikili kutambua deni hilo mara baada ya kubanwa na Shilatu juu ya upotevu huo.
"Sijaridhishwa na maelezo ya Mwenyekiti yamejaa ubabaishaji mwingi na kazi yetu Serikali ni kutatua kero za Wananchi wakiwemo wakulima ambao wanafanya kazi zao na hatutakubali jasho lao lichezewe. Hivyo nimetoa maelekezo viongozi hao wa Amcos wakamatwe mara moja." Alisema Shilatu wakati akizungumza na Mwandishi wetu.
Gavana Shilatu amewataka viongozi wa Amcos wenye michezo hiyo michafu waache mara moja na wahakikishe wamewalipa fedha zao Wakulima. Pia amewasihi Wananchi kuendelea kufanya kazi ipasavyo na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na viongozi wapo tayari wakati wote kulinda maslahi yao ili kila Mtu anufaike na jasho lake.

Mkulima, Fadina Hassan pamoja na Mwenyekiti Ngonda Amcos Rashid Lingoni wakiwa kituo cha Polisi cha wilaya Tandahimba kufuatia agizo la Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu aliyeagiza kukamatwa kwa uongozi wa bodi nzima ya Ngonda Amcos.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...